ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 1, 2012

BAMPA KWA BAMPA YA NEW YORK BAADA YA KUKUMBWA NA HURRICANE SANDY NA USAFIRI WA UMMA KUFUNGWA

New York City midtown.
Hali ya katikati ya jiji la New York traffic yake ni mbaya hii inatokana na kufungwa kwa usafiri wa umma na kutokana na miundo mbinu mingi kuathirika na hurricane sandy. Watu wakaamua kuendesha magari yao kuingia mjini kwa ajili ya kujitafutia riziki. New York kulikuwa hakuna shughuli yeyote iliyokuwa inaendelea watu wamekosa kufanya kazi kwa takribani siku 3 hadi 5 kutokana na sehemu nyingi kuharibiwa na kimbunga hicho na kusababisha kutokuwa na umeme na maji kuchanganyika na maji machafu na kusababisha kampuni husika kufunga maji kwa sababu za kiusalama na sehemu za kazi kufurika maji, majengo kubomoka na barabara kumong'onyoka huku miti ikiangukia majengo pamoja na magari pia kuangukiwa na miti hiyo kutoka na upepo mkali uliokuwa una vuma kwa 80 MPH (120 KM) idadi ya watu waliopoteza maisha mpaka sasa imefikia 61, hatujasikia chochote kama kati ya hao waliopoteza maisha yupo Mtanzania lakini kama tukipata chachote tutawataarifu mara moja.

Jumla ya galoni milioni 500 za maji yaliyopo mtaani na ndani ya nyumba za wakaazi wa jimbo la New Jersey, jitihada zinaendelea kuondolewa maji yote na kurudisha umeme ili maisha ya wakaazi wa jimbo hilo waliyoyazoea yarudi kama kawaida.

No comments: