Advertisements

Saturday, November 3, 2012

Bunda wamlalamikia Rais kwa rushwa kukithiri nchini


‘‘Kwa mfano, Rais angeonyesha mfano wa kumwajibisha Inspekta Jenerali wa Polisi kutokana na idara ya polisi kuongoza kwa rushwa, bila shaka wakuu wa idara zingine wangesimama kidete kuzuia rushwa’’, walisema

Mwandishi Wetu, Bunda
WAKAZI wa Jimbo la Bunda, katika Mkoa wa Mara wamesema kukithiri kwa vitendo vya rushwa nchini ni matokeo ya ukimya wa Rais Jakaya Kikwete na kumwomba achukue hatua kudhibiti kwenye idara mbalimbali.

Wakitoa maoni yao wakati wa mdahalo wa kujadili uwajibikaji na uwazi wa watumishi wa umma, uliofanyika leo katika Mji mdogo wa Nyamuswa jimboni humo, wakazi hao walisema ukimya huo wa Rais unatoa mwanya kwa wasiowaadilifu kuifanya rushwa kama sheria maeneo ya kazini na hivyo kupotosha haki.
Walisema kama Rais Kikwete angewafuatilia wanaolalamikiwa na kuwatolewa uvivu hadharani , watumishi wengi wangepatwa na woga na hivyo kuacha au kupunguza.

‘‘Kwa mfano, Rais angeonyesha mfano wa kumwajibisha Inspekta Jenerali wa Polisi kutokana na idara ya polisi kuongoza kwa rushwa, bila shaka wakuu wa idara zingine wangesimama kidete kuzuia rushwa’’, walisema. Mmoja wa wakazi hao, Charles Komanya alisema kukithiri kwa rushwa na ubinafsi miongoni mwa watumishi wa umma kumechangia kwa kiasi kikubwa kudorora kwa mfumo mzima wa haki katika jamii.

“Ubinafsi na rushwa vimesababisha kudorora kwa haki katika jamii. Watumishi na jamii kwa pamoja hawapati haki zao na hivyo kupoteza kabisa uwazi na uwajibikaji nchini,”amesema Komanya.

Aidha wakazi hao pia waliviomba vyombo vinavyohusika na masuala ya kisheria kutoa elimu ya uraia kwa wananchi maana wengi wakiwamo watumishii wa Serikali ngazi za vijiji na kata wanaonekana kutokujua
haki na wajibu wao hali inayopelekea wajanja wachache kutumia mwanya huo kujinufaisha kwa rushwa.

Mapema katika nasaha zake Katibu wa Mtandao wa ssasi za kiraia wilayani humo (Bunda Ngonet) alisema watumishi wengi leo hawawajibiki na kujituma kazini wala hawaonyeshi uzalendo kama
ilivyokuwa zamani na kuwataka watoe maoni yatakayoleta mabadiliko

No comments: