
Mmiliki huyo wa Chelsea, amekasirishwa na matokeo mabaya ya timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kumfukuza kazi Mtaliano huyo baada ya timu kuzabwa mabao 3-0 na Juventus jana, ikiwa ni miezi sita tu tangu aipe timu hiyo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Sasa mtu wa kwanza kabisa ambaye Abramovich anamtaka akarithi mikoba ya Mtaliano huyo ni kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola, na kama akikwama kwa Mspanyola huyo ambaye amesema hataki ukocha tena kwa sasa, basi atahamishia ndoana zake kwa Rafa Benitez.
MAKOCHA WALIODUMU MUDA MFUPI CHELSEA:
Guus Hiddink Siku 105
Felipe Scolari Siku 223
Avram Grand Siku 247
Andre Villas-Boas Siku 256
Roberto Di Matteo Siku 262
MATOKEO YALIYOMFUKUZISHA KAZI DI MATTEO:
Oktoba 23: Shakhtar 2 Chelsea 1 (Ligi ya Mabingwa)
Oktoba 28: Chelsea 2 Man United 3 (Ligi Kuu)
Oktoba 31: Chelsea 5 Man United 4 (Kombe la Ligi)
Novemba 3: Swansea 1 Chelsea 1 (Ligi Kuu)
Novemba 7: Chelsea 3 Shakhtar 2 (Ligi ya Mabingwa)
Novemba 11: Chelsea 1 Liverpool 1 (Ligi Kuu)
Novemba 17: West Brom 2 Chelsea 1 (Ligi Kuu)
Novemba 20: Juventus 3 Chelsea 0 (Ligi ya Mabingwa)
No comments:
Post a Comment