Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein
Na Salim Said Salim
Miaka mingi imepita, lakini ninakumbuka vizuri namna mchezo wa sinema ulioitwa “ Shane…look out”, yaani Shane angalia nje ulivyopendwa sana na vijana na wazee. Filamu hii ilipanda chati sambamba na “ filamu za Mother India”, “ One Silver Dollar” na “Ratoon Karaja”. Hii ilikuwa mwishoni mwa miaka ya 1950 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1960 na kufunikwa pale walipochomoza wacheza sinema wengine maarufu kama Clint Eastwood na filamu yake ya “Dirty Harry”.
Siku filamu ya mchezo wa “Shane look out” ilipoonyeshwa katika majumba ya sinema ya Zanzibar mji mzima wa Zanzibar ulitikisika. Mamia ya watu kutoka mashamba walifurika mjini kuiona kwa mara ya pili au ya tatu filamu hii.
Nyumba nyingi zilikumbwa na vilio vya watoto kutaka waze wao kuwapatia shilingi moja ya kununua tiketi ya sinema. Katika filamu hii, mcheza sinema maarufu wa Kimarekani wa zama zile, Allal Ladd, (alifariki miaka mine iliopita) alionywa na mtoto wa miaka 10 kutoridhika na mazingira aliyoyaona ndani ya hoteli.
Badala yake alimtaka kuwa muangalifu kwa kuangalia nje ambapo ndipo walikuwepo maadui waliohatarisha maisha yake. Katika watu ninaokumbuka kuupenda ya mchezo ule kutokana na ubabe uliokuwemo na sio mafunzo ya filamu alikuwa sahiba wangu wa karibu tokea tukiwa wadogo, Rais wa Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein.
Ninakumbuka mara nyingi tulipokuwa tunacheza mpira na alipokuwa anafukuzwa na mpinzani alipokuwa anakwenda kufunga goli nilikuwa nikimwambia “ Shein..look out”.
Leo mwenzangu akiwa kiongozi wa Zanzibar na mimi nikiwa na dhamana ya kutoa sauti a watu wasiosikika, wanyonge na wanaodhulumiwa ninamtahadharisha Mheshimiwa Rais kwa kumwambia :” Shein ..look out”, yaani Shein angali nje.
Ninafanya hivi kwa sababu mbali mbali. Kwanza kusema kweli hii ndio kazi yangu na pili kuelezea masikitiko ya wanyonge ni wajibu wangu, hata ikibidi kutofurahisha marafiki zangu.
Lakini la tatu ambalo kwangu lina umuhimu mkubwa ni kusaidia kulinda heshima, utu na uungwana aliokuwa nao tokea akiwa mdogo rafiki yangu, Rais Shein. Kwa jinsi tunavyojuana mimi siwezi kumdanganya Dk. Shein na yeye hawezi kunidanganya.
Ninaona muhali sana kumwambia:” Shein..look out”, lakini lisilobudi hutendwa. Kwa ninayoyaona Zanzibar hivi sasa ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kwamba hana habari kamili za hali inayoendelea . Ndio maana ninamtaka afanye juhudi za kujuwa huko nje ya Ikulu kuna nini?
Ukweli ni kwamba jhaki za binaadamu zinavunjwa kwa watu kupigwa ovyo na wengi na kuwa vilema na wengine kuuawa. Katika kuangalia huko nje angelianza na moja yasehemu anayoielewa vizuri sana, zaidi ya jingo la Ikulu. Nayo ni hospitali ya Mnazi Moha ambapo alifanya kazi kwa zaidi ya miaka 15.
Hapom akitembelea atapata maelezo ya watu wlaiopoigwa na hata kuvunjika viungo au kupata majeraha makali. Maeneo mengine anayostahiki kuyatemebelea na kuzisikia sauti za wanyonge ni pamoja naBububu, Daraja Bovu, Magogono, Kikwajuni, Jang’ombe na Kundemba.
Katika sehemu hizi watu wengi wameteseka, wengine pamoja na watoto wao wadogo.
Lawama juu ya uonevu huu wanashushiwa askari wa Jeshi la Polisi na vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kwa taarifa yake inasmeekana zipo picha na video ziliochukuliwa kwa siri pale maovu haya yalipofanyika.
Baadhi ya wakati askari hawa wanasemekana kuwa walikuwa wanajifunika nyuso zao, kama ninja, lakini watu wanadai kuwa wanawatambua waliowapiga na kuwatesa kwa sauti na mwenedo wao. Tukumbuke Zanzibar ni ndogo na watu wanajuana kwa majina, sura, mwendo au sauti.
Watu wanamuuliza Rais wao hivyo ni kipengele gani cha sheria kilichowapa askari polisi, Magereza au maofisa wa usalama wa taifa kuwanyoa ndeevu viongozi wa Uamsho. Au ndio kusema siku hizi watu wanahukumiwa Zanzibar hata kabla ya ye kesi zao kusikilizwa namahakama.
Wngine wanauliza kama askari wanayo haki kunyoa ndevu raia, jee na rai wanayo haki kuwanyoa nyewele askari polisi? Ukweli ni kwamba mengi yanasemwa mtani,a lakini liliokuwa wazi zaidi ni kuwa baadhi ya wananchi wameanza kupoteza imani kwa serikali yao.
Wapo piawanaouliza kuwa jee na wao watapewa haki ya kuwa namabango ya matangazo yanayotiukana, kukejeli na kukashifu watu kama zinavyoruhusiwa maskani za CCM. Au hio ndio kutekeleza ule msemo maarufu wa CCM wa “ Tunawatesa kwa zamu”.
Sahiba wangu Dk. Shein anapaswa kujuwa kuwa kwa kawaida binaadamu huzungumzwa na hata kuhukumiwa kwa maovu aliyoyatenda au kuyaridhia. Watu wana kawaida ya kusahau au kutoyajali mema ambayo mwenzao amefanya na humzumngumza au kumhukumu mtu kwa mabaya aliyoyatenda au kuyafumbia macho.
Zanzibar ilitulia sana baada ya Dk. Shein kuingia madarakani,lakini hali sivyo ilivyo hii leo. Hali hii sia ajabu pia ikaathiri sekta ya utalii ambayo ni mojaya mategemeo makuybwa ya kiuchumi ya Zanzibar.
Njia pekee za kuirekebisha hali ya hofu na vitisho viliotanda Zanzibar ni kwa kuunda tume guru ya uchunguzi na sio ya askari polisi au viongozi wa serikali ili ukweli wa mambo uwekwe wazi.
Lakini jengine muhimu ni kwa Rais kutoka nje na kupata taarifa kutoka kwa wananchi juu ya madai yao ya kupigwa mijeledi, kuteswa na kuporwa fedha na mali zao. Ndio maana ninamwambia tena Rais :” Shein look out”.
Kama kumbukumbu za ile filamu imempotea ni vizuri akaagiza apatiwe ili ajikumbushe umuhimu wa kuchukua tahadhari na kutoaamini wakati wote watu waliokuzunguka. Watub wengine katika jamii na hata katika serikali hutoa taarifa za uwongo ziliotiwa chumvi au sukari nyingi ili kuficha maovu yao na ya wenzao.
Mcheza sinema Allan Ladd aliangalia nje kama aliyoombwa na Yule mtoto na kuwaona maadui zake na kunusuru maisha yake. Ninaamini na Dk. Shein kama ataangalia nje sio tu atanusuru heshima aliyojijengea kwa miaka mingi kama daktari na mwana siasa ya kuwa mtu mpole, muadilifu , muungwana na mwana michezo mahiri, lakini pia atainusuru Zanzibar kupata maafa zaidi.
Tayari Zanzibar imepoteza watu wengi na wengine kuwa vilema kwa vipigo na mateso katika miaka ya nyuma na hasa zama za Ba-Mkwe. Wazanzibari hawataki kurudi nyuma na hawamtegemei Rais wao kuwapelaka huko.
Ninarudia kwa mara nyenine kumwambia sahiba wangu, Mheshimiwa Rais Dk.Ali Mohamed Shein: “Look out”.
No comments:
Post a Comment