
Aidha, amesema maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wale waliokuwa zamu siku shehena hiyo ikipitishwa bandarini Dar es Salaam kwenda Hong Kong, wanachunguzwa ili kubaini ukweli.
Alisema hayo wakati akifanya majumuisho ya hoja za wabunge waliokuwa wakijadili maazimio mawili ya Bunge kuhusu marekebisho ya mpaka na upanuzi wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe na lile la kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane.
“Hatuna uhakika bado kama meno yaliyokamatwa huko Hong Kong yana asili ya Tanzania au yalikuwa yakipitishwa nchini mwetu…tunafanya mazungumzo na balozi wetu kule China kuhusu suala hilo,” alisema.
Alisema taarifa ambazo zimekwishapatikana zinaonyesha kwamba kontena moja linatokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kontena lingine bado halijaeleweka wazi kwamba linatokea Tanzania au la, na ndio maana uchunguzi utahusisha vipimo vya DNA ili kujua asili ya meno hayo.
Oktoba 16, mwaka huu, maofisa usalama wa Hong Kong waliyakamata makontena mawili yaliyokuwa yamesheheni meno ya tembo yenye thamani ya dola za Marekani milioni 3.4.
Hata hivyo, kontena moja kati ya hayo lenye thamani ya dola za Marekani milioni 1.7 linadaiwa kuwa linatokea Tanzania.
Kama hiyo haikutosha, shehena ya meno ya tembo ilikamatwa bandarini Dar es Salaam Jumapili iliyopita na hali ambayo inaonyesha kasi ya kuuwa kwa tembo ni kubwa.
Mapema katika mchango wake binafsi, mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, alisema kuongeza mipaka ya hifadhi ni suala zuri lakini serikali inawajibu wa kulinda hifadhi hizo.
Alizungumzia tukio la hivi karibuni la kukamatwa kwa meno ya tembo huko Hong Kong na bandarini Dar es Salaam yanaashiria kwamba tembo waliopo kwenye hifadhi wanauawa.
“Hii inaonyesha jinsi gani tembo wetu wanavyoteketea,” alisema na kuongeza, “sifurahishwi sana kuona tembo wetu wanakufa.”
CHANZO: GUARDIAN ON SUNDAY
2 comments:
NPR(National Public Radio)walikuwa wanaelezea kuhusu tembo wa Tanzania wanavyouliwa wiki mbili zilizopita.Na wachina ndio huwa wanatoa oda za hayo meno.
Mh Waziri, hao wafanyakazi wa TRA waliokuwa zamu siku ya tukio wanapaswa kusimamisha kazi wakati uchunguzi ukiendelea.
Inatisha maana ripoti za kimataifa zinaonyesha kuwa Tanzania inaongoza kwa Tembo wake kuuwawa. Jamani tukisema hali ya Taifa letu "lenye amani"
inakwenda pabaya kwa rushwa na ufisadi tutakosea??.Viongozi mlio madarakani tTIMIZENI wajibu wenu na Raia wema....IF YOU SEE SOMETHING< SAY SOMETHING (ukiona kitu usinyamaze..sema)
Post a Comment