
MAJANI/ MATUNDA
Kundi la pili ni mboga za majani na matunda. Ni wajibu wa kila mtu kula matunda na mboga za majani kwa wingi kila siku ili kujenga na kuimarisha kinga ya mwili.
Hivyo, suala la kula matunda na mboga mboga siyo anasa, bali ni jambo la lazima kwa mwili wa binadamu.
MAZIWA
Kundi linalofuatia kwa umuhimu ni la vyakula vitokanavyo na maziwa na bidhaa zake zote kama mtindi, samli, siagi, jibini, n.k. Ulaji wa vyakula vya kundi hili ni wa kiasi tofauti na ule wa kundi la kwanza na la pili tuliyoyataja hapo juu.
NYAMA /SAMAKI
Kundi la tatu ni lile la vyakula vya nyama, samaki, maharage na vingine vinavyoongeza protini mwilini. Ulaji wa vyakula vya kundi hili ni wa kiwango kidogo sana, kwani ni kundi lenye vyakula hatari kama vikiliwa kupita kiasi.
MAFUTA, SUKARI
Kundi la mwisho ni kundi lenye vyakula vya mafuta na sukari. Vyakula vya kundi hili vinatakiwa kuliwa kwa kiasi kidogo sana kuliko makundi yote. Ulaji wa vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi ni hatari sana kwa afya ya mlaji.
Kwa kifupi, huo ndiyo muongozo wa vyakula unaotakiwa kufuatwa na kila mtu ili kuwa na afya bora, lakini katika hali halisi ya maisha, muongozo huo umebadilishwa na kuwa chini – juu.
Vyakula vinavyotakiwa kuliwa kidogo ndivyo vinavyoliwa kwa wingi na vile vinavyotakiwa kuliwa kwa wingi, vinaliwa kwa uchache au haviliwi kabisa.
Hilo ndiyo kosa Kubwa tunalolifanya ambalo ndiyo chanzo cha magonjwa hatari yanayotukabili sasa.
MAJI
Mwisho, maji nayo ni muhimu kuliko kitu chochote, kila mtu anatakiwa kunywa maji mengi kila siku, iwe amesikia kiu ama la. Kiwango cha chini kabisa cha maji ni glasi nane kama huna kazi nzito.
Ni kosa Kubwa kutokunywa maji na dalili za kutokunywa maji huonekana pale unapoenda haja ndogo kwani haja huwa nyekundu na yenye harufu kali.
Hivyo basi, tunashauriwa kunywa maji mengi kila siku ili kusafisha na kuondoa sumu mwilini inayoingia kutokana na vyakula tunavyokula, kwa kuwa na utaratibu huu ndipo mtu unapoweza kuwa na afya njema na imara.
MWISHO.
Chanzo: www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment