ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 11, 2012

JK ACHARUKA DODOMA


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ccm Rais Jakaya Kikwete amekemea tabia inayofanywa na wanachana wanaogombea uongozi ndani ya chama kuacha mara moja kuendekeza malumbano yasiyo na tija kwani kufanya hivyo kunakifanya chama kudhoofika miongoni mwa wanachana na wananchi kwa ujumla.
Rais Kikwete amekemea hali hiyo leo wakati akifungua mkutano mkuu wa nane wa chama unaofanyika katika ukumbi wa kizota nje kidogo ya mji wa dodoma.

rais kikwete amekemea hali hiyo kufuatia kuwepo kwa malumbano yanayoendelezwa na wagombea ambao makundi yao yanafanya chama kielelweke vibaya kwa wananchi.
kwa sababu hkiyo amewataka wananchi hususani wanachama kuwafichua wagombea au viongozi viongozi wa aina hiyo ili wachukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kuondolewa ndani ya chama kwani chama kinataka viongozi wanaozingatia uaminifu na umakini katika utekelezaji wa majukumu yao.

Hata hivyo Rais Kikwete katika hotuba yake iliyochukua muda wa saa tatu amesema chama hakipo tayari kuona viongozi wake wanakuwa na ndimi mbili huku wakikisema vibaya chama hivyo hawapashwi kugombea au kuwa viongozi ndani ya chama tawala.

pamoja na mambo mengine, rais kikwete amesema viongozi wa namna hiyo lengo lao ni kukiua chama tawala, hivyo wanachama wasisite kuwafichua au kutowaunga mkono ili kukomesha hali hiyo.
katika hatua nyingine, amewahakikishia wananchi kuwa mipaka ya nchi ipo imara licha ya changamoto kadhaa zinazojitokeza ikiwemo ya malumbano kuhusu mpaka wa ziwa nyasa na vurugu zilizojitokeza katika maeneo kadhaa  maeneo nchini.

pia amewataka wananchi hususani wanaccm kutembea kifua mbele kutokana na kutekelezwa kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi katika nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara.

No comments: