Joseph Lyimo,Hanangí
TATIZO la muda mrefu la uhaba wa maji katika mji mdogo wa Katesh, wilayani Hanangí limepatiwa ufumbuzi baada ya Rais Jakaya Kikwete kuagiza Hazina itoe Sh395 milioni, ili kufanikisha mradi wa maji kwa wakazi wa mji huo.
Rais Kikwete alisema hayo juzi baada ya Mhandisi wa maji wa wilaya hiyo, Sultan Ndoliwa, kumweleza kuwa fedha hizo zinahitajika ili kuwezesha utekelezaji wa mradi huo.

Mhandisi huyo alisema kwa Serikali kiasi hicho ni kidogo na kwamba ni matarajio yake kuwa kitatolewa, ili kuwawezesha wananchi kuondokana na adha ya kukosa huduma za maji.
Ndoliwa alisema mahitaji ya maji kwa wakazi wa eneo hilo ni lita 1,965,000 kwa siku lakini kwa sasa wanapata maji kiasi cha lita 1,130,000 cha maji kwa siku.
Alielezea matumaini yake kuwa fedha hizo zikitolewa, mradi huyo unaweza kukamilika ndani ya miezi mitatu na hivyo kuwafanya wananchi kupata huduma za maji.
Mapema, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Felix Mabula, alisema mradi huo wa maji ulitolewa kutoka katika eneo la Mogitu, kilometa saba kutoka Katesh, lengo likiwa ni kumaliza kero ya maji ya muda mrefu kwa watu wa eneo hilo.
Mabula alisema walifanikiwa kuchimba visima 33 virefu na vingine 12 vifupi na kwamba nane vinafanyakazi.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya hiyo, Christine Mndeme, alimshukuru Rais Kikwete kuwezesha ujenzi wa Barabara ya Minjingu-Babati na Katesh-Singida, ambayo itawarahisishia wananchi usafiri.
Akizungumza juzi mjini Katesh wakati akihitimisha ziara yake mkoani Manyara, Rais Kikwete alisema ametimiza ahadi yake ya ujenzi wa barabara kwa wananchi wa eneo hilo.
Nilifika pale (Katesh) wakaniambia nisiseme chochote wenyewe wanahitaji barabara ya lami kwani wamechoka na vumbi, linawaathiri na barabara ndiyo hiyo nimeshaikamilisha na kuwatimiza ahadi yangu kwenu,î alisema Rais Kikwete.

Mwananchi
No comments:
Post a Comment