Advertisements

Friday, November 30, 2012

Maalim Seif aongoza mamia kumzika mke wa Hamad Dar

Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la marehemu Kissa Gwalugano Mohamed,ambaye ni mke wa Mbunge wa Wawi,Zanzibar Bw.Hamad Rashid Mohamed,kwenda msikitini na mazishi kufanyika jana jioni katika makaburi ya Kisutu,Dar es salaam.
Na Goodluck Hongo

MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, jana aliongoza mamio ya waombelezaji katika mazishi 
ya Kissa Gwalugano Mohamed ambaye ni mke wa Mbunge wa 
Wazi, Zanzibar Bw. Hamad Rashid Mohamed.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Pamoja na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Bw. Wiliam Lukuvi, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Ludovick Utouh.


Wengine ni Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa UDP, Bw. John Cheyo, viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa pamoja na wabunge.

Katika msiba huo, viongozi wa kisiasa waliweka pembeni tofauti zao na kumfariji Bw. Mohamed ambaye chama hicho kiliwahi kumfukuza uanachama.

Mazishi hayo yalifanyika Dar es Salaam jana katika makaburi ya Kisutu, saa kumi jioni.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Profesa William Matuja aliwashukuru viongozi wote walioshiriki mazishi hayo kwani wamefarijika sana ingawa wamepata pigo kwa kifo hicho.

Marehemu alizaliwa Oktoba 20,1955 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, alisoma katika Shule ya Msingi Azimio, baadaye Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam.

Alisema baadaye alijiunga na masomo ya kompyuta na kuajira THB (iliyokuwa Benki ya Nyumba nchini), lakini alichana kazi na kuamua kujiajiri mwenyewe hadi mauti ilipomkuta.

Alifunga ndoa na Bw. Mohamed mwaka 1984 na walibahatika kupata watoto kati ya hao mmoja wa kiume. Marehemu alikuwa akilalamika kusumbuliwa na mgongo na baada ya kupimwa 
iligundulika kuwa na ugonjwa wa mifupa.

Marehemu alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Novemba 27 mwaka huu, baada ya kuzidiwa na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kufariki saa tatu usiku.

Majira

1 comment:

Anonymous said...

Jamani kuna ugonjwa wa mifupa ndiyo nini?? Arthritis?? OMG pole Uncle kwa msiba huu mkubwa jamani, she is too young to die. Yale yale ya seriously viongozi wetu mnahitaji kureview the health system in Tanzania. Just this week nimesoma habari za kusikitisha kuhusu vifo vya vijana ambao na uhakika vimesababishwa na UZEMBE WA MADAKTARI FOR NOT GIVING PROPER DIAGNOSIS OR PROPER TREATMENT.