Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige, akiwa na baadhi ya vijana wakibadilishana mawazo kabla ya uzinduzi uliokwenda sambamba na sherehe ya uzinduzi wa Catherine Development Foundation Limited kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha leo Asubuhi pamoja na kutoa msaada wa baskeli kwa walemavu wa wilaya ya Arusha.
Mheshimiwa Catherine Magige, akijadili jambo kabla ya kuanza kwa hafla ya kutoa misaada ya baiskeli kwa walemavu na kuzindua mfuko wake wa misaada na maendeleo wa Catherine Development Foundation Limited.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela, akisalimiana na baadhi ya wageni waliohudhuria.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela (kushoto) na Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), Mkoa wa Arusha, wakiwa meza kuu kabla ya kuanza kukabidhi misaada kwa walemavu.
Mbunge wa viti maalum bi Catherine Magige akisoma taarifa ya mfuko wake, kuhusu nia na malengo pamoja na jinsi ilivyoanza kazi mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela na wananchi wengine waliohudhuria.
Baadhi ya walemavu waliopata msaada wa baiskeli kutoka kwa Catherine Development Foundation Limited. Nyuma ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela na Catherine Magige.
Baadhi ya walemavu waliopokea misaada ya baiskeli na wageni waliohudhuria hafla hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge Catherine Magige na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Maongela.
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha kwa tiketi ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Catherine Magige, leo amejenga matumaini kwa walevu 20.
Catherine, aliwapa msaada wa baiskeli za kisasa walemavu hao ambayo kila moja imegharimu shilingi 300,000 ambazo jumla yake ni shilingi 6,000,000.
Pamoja na msaada huo kwa walemavu hao, Catherine pia aliitumia siku ya leo kuzindua mfuko wako wa kusaidia wanawake na watoto unaoitwa Catherine Development Foundation Limited.
Shughuli hiyo, ilifanyika leo asubuhi kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, jijini Arusha na kuhudhuriwa na watu wa kada mbalimbali.
Baadhi ya walemavu, wakizungumza kwa niaba ya wenzao, walimshukuru Catherine kwa msaada huo, kwani viti hivyo ni vya kisasa.
Sifa nzuri ya viti hivyo ni kuwa vina mito ya kukali ambayo humfanya anayekalia kutopata maumivu yoyote hata kama atakaa kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Catherine alisema kuwa misaada hiyo ni mwanzo tu, kwani mfuko wake wa Catherine Development Foundation Limited utafanya mambo makubwa sana katika kusaidia tabaka la watu wenye kuhitaji.
Misaada hiyo, inakuwa mwendelezo wa matukio ya Catherine kuisaidia jamii, kwani huko nyuma ameshatoa misaada mingi kabla hata hajaanzisha mfuko huo wa misaada na maendeleo.
Baadhi ya misaada ni baiskeli kwa walemavu na mitaji ya biashara kwa vikundi vya wanawake wa Wilaya za Longido na Arumeru, kutoa misaada ya ofisi za UVCCM na UWT, Longido, Arumeru na Mkoa wa Arusha na kuwalipia faini wafungwa waliokuwa jela baada ya kushindwa kulipa faini walizohukumiwa.
Catherine pia alimsaidia mwanamke mwenye tatizo la kuzaa kimiujiza, vilevile alitoa misaada kwa timu za mpira wa miguu mkoani Arusha na kadhalika.
No comments:
Post a Comment