ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 19, 2012

MKUTANO WA MAPOKEZI YA MWENYEKITI NA SEKRETARIETI MPYA YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Meza Kuu wakati wa mkutano wa mapokezi ya Mwenyekiti pamoja na Sekretarieti Mpya katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Baadhi ya wana-CCM wakifuatilia mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa kwa ukakamavu.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya mnazi mmoja, ambapo yamefanyika mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Sekretarieti Mpya iliyoundwa baada ya Mkutano Mkuu wa Chama uliofanyika hivi karibuni katika Mji wa Dodoma.

Mkutano huo ambao huko chini ya Mkoa wa Dar es salaam ambao unafanya sherehe za mapokezi ya viongozi wapya waliochaguliwa na kupitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kuwa safu mpya ya kukisimamia, kukiimarisha na kukiendeleza Chama hicho.

Mkutano huo ambao ulianza majira ya mchana wa saa nane na kumalizika saa kumi na mbili ulitawaliwa na matukio mbalimbali zikiwemo hotuba muhimu kutoka kwa viongozi hao wapya ambao walisisitiza kuwa sasa kikosi kamili kimetimia na yale ambayo yalikuwa yanawakwaza wanaCCM likiwemo suala la Rushwa katika chaguzi, upendeleo na kupanga safu ya uongozi kwa maslahi binafsi, Katibu Mkuu wa Chama Hicho alisisitiza juu ya Kuondoa kabisa tatizo la UBINAFSI ambalo ndio chanzo kikubwa cha makundi na migogoro katika chama hicho.

1 comment:

Anonymous said...

Safu ya Mazishi ya CCM