Mwandishi Wetu, Zanzibar
MTUHUMIWA anayedaiwa kuimwagia tindikali familia moja Zanzibar ametiwa mbaroni na polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo mjini hapa.Mtu huyo (jina lnahifadhiwa) jana alikuwa Kituo cha Polisi cha Bububu, Mkoa wa Mjini Magharibi anakoshikiliwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma Mohammed alithibitisha kwa njia ya simu juzi kutiwa mbaroni kwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akisakwa kwa zaidi ya miezi miwili.
Kamanda Aziz alisema kwamba mtuhumiwa huyo, alikamatwa Jumapili iliyopita Bandarini jijini Dar es Salaam na aliletwa Zanzibar juzi.
Kamanda Aziz hakupatikana jana, lakini habari za Polisi zinasema kwamba mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo baada ya kufanyiwa mahojiano na polisi jana.
Mtuhumiwa ambaye ni maarufu anadaiwa kuimwagia tindikali familia moja na kuwadhuru watu sita na kutoweka hadi alipotiwa mbaroni Dar es Salaam.
Watu sita wa familia hiyo inayoishi Silver Bububu jirani na mtuhumiwa ambao walidhurika katika shambulio hilo ni Salim Ali Abdallah, Suleiman Azzan, Sabra Amour Said, Husna Amour Said, Ghaniya Suleiman Azzan na Azzan Suleiman Azzan.
Tukio hilo lilitokea Sepetemba 5, mwaka huu na hivi karibuni watu wasiojulikana walimmwagia tindikali Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Suleiman Soraga na hivi sasa yuko India kwa matibabu.
Mwanannchi
No comments:
Post a Comment