ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 14, 2012

NASSIBU RAMADHANI NA FRANSIC MIYAYUSHO KUGOMBANIA UBINGWA WA WBF DESEMBA 9

Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam 
Mwandaji wa mpambano wa ubingwa wa WBF Mohamed Bawazir katikati akiwa ameshika mkanda na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Fransic Miyayusho kulia wengine kulia ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa ambao na wasimamizi wa mpambano huo na Kushoto ni Mratibu Paul Kunanga na Kocha wa Nasibu Christopher Mzazi
Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam 

KAMPUNI YA Darworld Links imeandaa mpambano mwingine wa ubingwa wa masumbwi utakaowakutanisha bondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho mpambano utakaofanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mohamed Bawazir

Amesema amewakutanisha mabondia hawo kutaka kujua nani zaidi ya mwenzake kwa kuwa viwango vyao vina fanana na vinatambulika kimataifa hivyo amewataka watanzania kujitokeza kuwapa sapoti hususani kudhamini mchezo huo wa masumbwi ata kwa bondia mmoja mmoja kuwagea changamoto mbalimbali mabondia hawa vijana wana uwezo mkubwa wa kutangaza biashara mbalimbali kupitia mchezo wao wa masumbwi kwani makampuni mengi yamekuwa yakiupiga danadana mchezo huu ni mchezo kama michezo mingine nashangaa sana kuona tunakosa

Udhamini tunapoomba sehemu ya makampuni mbalimbali ukienda wanasema atuhusiki na mchezo huo

Wengine wanasema kabisa wadhamini wa michezo wakati wanabagua michezo mingine kama ngumi awapewi kipaumbele kabisaa

amewaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza siku ta 9 Desemba kuja kuangalia ngumi ili zisonge mbele 
watakaosindikiza mpambano huo wa masumbwi ni 
Fadhili Majia VS Juma Fundi
Moh'd Rashid Matumla VS Doi Miyayusho
Ibrahimu Class 'King Class Mawe' VS Said Mundi wa Tanga
Fred Sayuni VS Deo Samweli
Hassani Kidebe VS Baina Mazola

Mapambano yote ya utangulizi ni mazuri na vijana wanaotakiwa kuendelezwa katika elimu ya masumbwi Duniani ili wawe mabondia wazuri 

Mpambano huo umedhaminiwa na JB BELMONT HOTEL gazeti la Jmbo Leo, Times FM

Na wengine wameobwa kujitokeza katika udhamini huo kwa mawasiliano zaidi 
0716 332933
0784 426542
KWA AJILI YA KUTOA SAPOTI YA AINA YOYOTE PAMOJA NA USHAULI KATIKA MPAMBANO HUU

No comments: