Kijana wa kikristo alimuuliza kijana wa kiislam,"kwa nini wanawake wa kiislam wanavaa nguo kufunika miili yao na vichwa vyao?",kijana wa kiislam akacheka kisha akachukua pipi mbili ya kwanza akaitoa nailoni inayoiziba ya pili akaiacha na nailoni yake kisha akazitupa kwenye vumbi na kumuuliza kijana wa kikristo "Ipi kati ya hizi pipi utaichukua?" kijana wa kikristo akasema "hiyo yenye nailoni" kijana wa kiislamu akamuuliza "kwa nini?" kijana wa kikristo akajibu "kwa kuwa haijachafuka na vumbi" kijana wa kiislamu akamwambia "basi hivyo ndivyo uislamu unavyomthamini mwanamke!"
5 comments:
Kaka umefika kwenye utani wa dini tena....mambo ya imani haya hayaitaji utani.
Khamis
Chicago
Nakushauri uachane na haya mambo ya utani wa namna hii yatakuharibia blogu.
Mdau,
Kansas.
Utani wa dini si mahali pake hapa.
Mpwa...asante sana kwa huu ujumbe mimi ni mwanamke wa kiislam na sivai hijaab lakini huu ujumbe kama umenikumbusha umuhimu wa mwanamke wa kiislam kuvaa hijaab. Asante sana mungu akubarik kwa hili tafadhali endelea kufanya kazi yako nzuri.
Sio mbaya sana
Post a Comment