ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 16, 2012

Walalamikia wake wa vigogo kufundisha shule za mijini

BAADHI ya wanafunzi wa shule za msingi  na sekondari  mkoani Lindi, wameulalamika  utaratibu wa mgao wa walimu ambao wake za vigogo na walimu wenye sifa, wanarundikwa katika shule za mijini.
Utaratibu huo unasababisha kukosekana kwa uwiano katika utaoji wa elimu baina ya shule za mijini na vijijini.
Wanafunzi hao walitoa malalamikoa hayo juzi kupitia katika Baraza la Watoto la Wilaya ya Kilwa, alilipokuwa likizungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea mabaraza hayo  kwa  ufadhili wa Shirika la Save the Children.
Akizungumza kwa  niaba ya baraza la watoto la wilaya hiyo, Idrisa  Samli,  alisema moja ya  kero na sababu zinazochangia  kuzohofisha morali ya watoto kutopenda shule, ni pamoja na kitendo cha watendaji na viongozi  wa halmashauri  hiyo, kutoa upendeleo kwa ndungu na wake zao, kufundisha shule za mijini.
Samli alisema kitendo hicho  ndiyo chanzo cha kukithiri kwa tatizo la utoro miongoni mwa wanafunzi na tofauti katika uatoaji wa elimu kati ya shule za mjini na vijiji .
Alielezea kushangazwa kwake kuona viongozi wa elimu katika wilaya hiyo, hawalichukulii suala hilo kama sehemu ya matatizo yanayochangia kushusha  kiwango cha taluuma.
Baraza hilo limeuomba uongozi wa wilaya,  kuangalia uwezekano wa kuwapunguza walimu wanaofundisha  mijini na kuwapeka vijiji ambako kuna  upungufu mkubwa wa walimu.
Limesema hatua hiyo itasaidia kuleta wiano wa walimu na wanafunzi katika shule za mijini na vijijini.

No comments: