MKAZI wa Kata ya Nyakabindi wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu, Paul Sanungu ametaka katiba Mpya ifute mwenge wa uhuru kwani unalipa taifa hasara.
Sanungu akizungumza katika mkutano wa kutoa maoni ya kuundwa kwa Katiba Mpya, alisema mbio za mwenge wa uhuru zinatumia fedha nyingi za umma, lakini hauleti manufaa yoyote.
Kwa upande wake Martin James mkazi wa kata hiyo, alisema katika Katiba Mpya asasi za kiraia na waandishi wa habari, watambuliwe kuwa ni mhimili wa nne wa dola.
Alisema pia kuwa tume ya Nyalali ilipendekeza sheria 40 kandamizi ambazo mpaka sasa zimesahaulika, hivyo Katiba Mpya ihakikishe mapendekezo hayo yanafanyiwa kazi.
Alisema pia kuwa tume ya Nyalali ilipendekeza sheria 40 kandamizi ambazo mpaka sasa zimesahaulika, hivyo Katiba Mpya ihakikishe mapendekezo hayo yanafanyiwa kazi.
Alieleza pia kuwa sheria ya ardhi ya mwaka 2009, inayosema mtu akikaa sehemu kwa muda wa miaka 12 ardhi hiyo ni yake, ifutwe.
“Mtu umemkaribisha ili ajitafutie maisha sasa akikaa miaka 12 anakwambia ardhi ni yake, inatakiwa hiyo sheria ifutwe,” alisema.
1 comment:
haya haya tena fungukeni haya tungeyasema sisi wazanzibari tungeambiwa wa dini sasa haya yanatoka kwenu mungu alishasema toka zamani katika maandiko yake matakatifu kwamba panapo ukweli au ukweli ukidhihiri uongo unajitenga daima uongo hauna mashiko hata siku mmoja pamoja na dhulma.
sasa tuambiyeni huyu jama wa mkoa wa simiyu wilaya ya bariadi ni mzanzibari au mpemba asiye au mpemba asiye utaka mwenge?
ukweli unajidhihirishia na bado
Post a Comment