ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 13, 2012

HAPA NA PALE KATIKA PICHA

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanazuoni, mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 
Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam jana, kinachojadili jinsi ya kuwawezesha Watanazania
kuongeza kipato na kukuza uchumi wao kwa maendeleo. (Picha na Anna Titus)
Baadhi ya wanawake wachuuzi wa ndizi wakivuka reli eneo la KAMATA, Dar es Salaam jana, wakati wakiwa katika harakati za kusaka wateja. Biashara hiyo inapendwa na wanawake wenye kipato kidogo kutokana na kutohitaji mtaji mkubwa. (Picha na Charles Lucas)
Bw. Mussa Chilungo akiwa katika moja ya vipindi vya Redio katika kituo cha Redio cha Halmashauri ya Ruangwa mkoani Lindi (kushoto) ni mtangazaji mwenzake Janethy Msangula)
Mkazi wa jiji akimuuzia, dereva teksi maji yaliyofungwa katika mifuko ya plastiki, kama walivyokutwa Mtaa wa Mhonda, Dar es Salaam jana. Baadhi ya watu wamekuwa wakitumia maji yanayouzwa mitaani bila kujua vyanzo vyake kwa usalama wa afya vyao. (Picha na Charles Lucas)
Marobota yenye bidhaa za wafanyabiashara wenye maduka yakiwa katika Barabara ya Mtaa wa Kongo Kariakoo, Dar es Salaam jana. Utaratibu huo unasababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara hiyo. (Picha na Charles Lucas)

Mawakala wa kuzoa takataka wakitwikana mfuko wenye chupa tupu za plastiki ambazo huziuza na kujiongezea kipato, kama walivyokutwa na mpiga picha wetu makutano ya Barabara ya India, Dar es Salaam jana. (Picha na Prona Mumwi)
Mbeba mizigo wa Mtaa wa Kongo Jijini la Dar es Salaam, akijitwika bidhaa za wateja baada ya kukodiwa, kama alivyokutwa jana. (Picha na Prona Mumwi)

No comments: