MPENZI wa safu hii, leo naendelea kutiririka na makala haya niliyoanza wiki iliyopita, hebu tuwe pamoja ili ujifunze kitu kuhusiana na kulilinda penzi na kuachana na mpenzi king’ang’anizi...
LAKINI KUNA RAFIKI MSEMA OVYONimekutolea mifano juu na umeona. Umejiridhisha kuwa pamoja na kasoro zake bado anastahili kupewa hifadhi ya moyo wako. Lakini kuna huyo anayekwambia uachane naye. Je, unampa nafasi gani?
Jibu unalo, lakini kwangu nikikushauri kitaalamu kama muongozo ni kuwa unatakiwa uangalie moyo wako unakupa jibu gani kuliko kusikiliza anachosema rafiki. Ujazo wake kwenye moyo wako haujui na hatambui ni kiasi gani utaathirika ukimkosa.
Je, rafiki anakuja na hoja au ngonjera? Anaponda badala ya kukupa njia ya kufanya. “Ooh, achana naye, kwanza yule malaya sana atakuua.” Somo hili likupe sababu ya kuwaona marafiki wenye uelewa wa hisia kwa sababu utakapokosa usingizi usiku kwa sababu ya mawazo hatakuwepo.
Kama mwenzi wako hafai au anafaa, jibu lipo ndani ya kuta za moyo wako. Ndiyo maana linapokuja suala la kupokea ushauri wa kimapenzi, unatakiwa umuone mtu ambaye ana sifa ya kutoa ushauri. Tafuta washauri na siyo wapondaji.
Unaweza kuwaazima masikio marafiki zako, wakampaka mwenzi wako badala ya kukupa ufumbuzi wa kile kinachokusumbua. Mwisho ukaona yao ni mazuri halafu kwa hasira ukachukua uamuzi wa kuachana naye, utajuta baadaye. Itakutesa zaidi baada ya kubaini kuwa mmoja wa waliokuwa wanamponda ndiye kamchukua.
Nimekuwa nikilieleza hili mara kwa mara kwamba mapenzi yanapoangaliwa kila upande, unakuja kupata jibu kwamba hakuna uhusiano uliokamilika. Muhimu kwako ni kumkubali mwenzi wako kama alivyo na kumpa heshima yake ya asimilia mia moja.
Kumkubali ni kutambua ujazo wake moyoni mwako. Hapa nikiwa na maana kwamba wewe mwenyewe unakuwa umejiridhisha kuwa unampenda kwa alama zote, hivyo umeamua kufanya naye maisha.
Uvumilivu unahitajika kwa kila mmoja, lakini busara iliyo wazi ni kwamba hutakiwi kuishi kwa kutazama makosa ya mwenzi wako. Mwisho wa siku naye ni binadamu, kwa hiyo unaishi na kiumbe chenye damu na moyo, siyo malaika.
Unashauriwa kumtambua mwenzi wako kwa jinsi alivyo na kujua namna ya kurekebisha kasoro zake. Uwe wa kwanza kujua udhaifu wake na kumkosoa kwa vipimo, siyo kwa sababu Mungu amekujalia mdomo na sauti ndiyo kila siku upayuke.
Una kila sababu ya kuzungumza na kutaka ushauri kuhusu mwandani wako lakini siyo nidhamu ‘kumvua nguo’. Hapa napitisha hoja kuwa kutoa kipaumbele kwa mwenzi wako ni sehemu ya nidhamu ya kimapenzi.
Wiki iliyopita nilikuonesha mifano. Unatakiwa ujiridhishe mwenyewe kuwa pamoja na kasoro zake bado anastahili kupewa hifadhi ya moyo wako. Lakini kuna huyo anayekuambia uachane naye. Je, unampa nafasi gani?
Jibu unalo, lakini kwangu nikikushauri kitaalamu kama muongozo ni kuwa unatakiwa uangalie moyo wako unakupa jibu gani kuliko kusikiliza anachosema rafiki. Ujazo wake kwenye moyo wako haujui na hatambui ni kiasi gani utaathirika ukimkosa.
Je, rafiki anakuja na hoja au ngonjera? Anaponda badala ya kukupa njia ya kufanya. “Ooh, achana naye, kwanza yule malaya sana atakuua.” Somo hili likupe sababu ya kuwaona marafiki wenye uelewa wa hisia kwa sababu utakapokosa usingizi usiku kwa sababu ya mawazo, hatakuwepo.
Itaendelea wiki ijayo

No comments:
Post a Comment