ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 18, 2012

MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHADEMA KILICHODUMU SIKU 2 MFULULIZO JIJINI DAR


Mwenyeketi wa Chadema Taifa, Mhe.Freeman Mbowe akiongea na wanahabari leo (hawapo pichani).
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa akiwa katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea leo.
kwa picha zaidi bofya read more
Sehemu ya wanahabari waliohudhuria mkutano huo leo.
Picha kwa hisani ya MJENGWA BLOG
---
Haya ndiyo tuliyoazimia kama kamati kuu ya chama, kikao kilichodumu kwa siku mbili mfululizo hapa jijini Dar es salaam,
1.KIKAO cha kamati kuu kilikuwa cha kawaida, hakuna jambo la dharula.
2.Mchakato wa katiba mpya usiathiri mabadiliko ya sheria nyingine kama mabadiliko ya sheria ya uchaguzi.
3.Mwaka 2013,ni mwaka wa nguvu ya umma,hakuna kubembelazana na serikali rais kikwete hajajibu madai ya yetu kwa hiyo tutamshinikiza.
4.Sehemu ambazo CCM wanaogopa kuitisha uchaguzi,tutawalazimishwa kuitisha uchaguzi kata za arusha mjini, Sengerema, nk. ziko 15.
5.Uongozi wa KARATU wa CHADEMA Tumeusimamishwa kwa muda mpaka chama kitakapokamilisha uchunguzi wake
huko wanasheria Marando na Prof Safari watachunguza kashfa za mtu mmojammoja huko karatu, kumekuwa na kashfa kwenye
miradi ya maji na ardhi.
6.Hatua za kisheria kufuatia matukio ya uchaguzi wa ilemela mwanza, baada ya madiwani 2 kufukuzwa uanachama
zitaendelee kuchukuliwa,pia hatua za kisiasa zianzishwe kudai uwajibikaji wa halmashauri ya jiji la mwanza ili haki itendeke.
7.Kamati kuu imetambua kutapatapa kwa CCM juu ya sera zake za katiba mpya, elimu bure na bei ndogo za vifaa vya ujenzi CCM haiaminiki,kwa hiyo CHADEMA tutaendelee kuunganisha umma ili CCM iondolewe 2014 na 2015.
8. M4C itaendelee kwa kasi mapema mwaka 2013,sekretariati itatangaza ratiba januari.
9.Juu ya hoja binafsi za wabunge wetu zito na mdee(kuhusu uporaji wa ardhi na mabilioni ya Uswis), pamoja na hoja ya Tundu Lisu juu ya uteuzi holela wa rais wa majaji,kamati kuu imependekeza maazimio ya bunge yafuatwe na baadaye kidogo kama hairidhiki kamati kuu itaelekeza nini kifanyike kwa hatua za ziada
10.Kamati kuu imesikitika kuwa rais amepuuza barua ya yetu juu ya kuunda tume ya kimahakama kuhusu mauwaji mbalimbali nchini.hivyo M4C itatumika mwaka 2013 kumshinikiza rais kujibu barua hiyo na kutekeleza yale barua inaelekeza yafanyike
Kamati kuu imesisitiza kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma na hakuna tena kubembelezana na serikali.
Sisi kama chama tunatambua mchango wenu sana, kwa pamoja tutapata mabadiliko tuyatakayo.
Kiongozi wenu
Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)

No comments: