ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 10, 2012

Msiba wa Baba Mzazi wa mwanajumuiya Grace Mwasokwa. Harlem , New York.]


Mzee Joseph Mwasokwa 
Wanajumuiya,Tunasikitika kutangaza kifo cha Mzee Joseph Mwasokwa (72), Baba mzazi wa dada yetu Grace Mwasokwa amefariki Jumamosi Desemba 9th, 2012 usiku nje ya geti la nyumbani kwake,mjini Mbeya. 
Ni Mstaafu wa usalama wa Taifa. Atazikwa Jumanne Desemba 11, 2012 kijijini kwake Kyela. Ameacha Mjane, watoto 7 na wajukuu. Alikuwa mpenzi sana wa soka na timu ya Yanga. Mwenyezi Mungu aipokee roho ya Marehemu na ailaze mahala pema -Amin.

Kama ilivyo adha yetu tunaombwa sote kwa umoja wetu na upendo tufike kwa Dada Grace kumpa pole na kutoa ushirikiano wetu wa kiroho na wa dhati katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo ya Baba yetu mpendwa!

Address: 2855 8th Avenue apt. 2C
New York, NY 10039 (Harlem)
btn 152nd & 153rd Street on 8th Avenue (Frederick Douglas Avenue)- Harlem
Tel. (347)422-3297 au (347)712-8539
"Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina”
Raha ya Milele Umpe Eee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazie apumzike kwa amani. Amina

Shabani Mseba
The Secretary i.e

No comments: