ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 24, 2012

Tunajiandaa kumpeleka Slaa Ikulu- Heche


Dr. Slaa

MWENYEKITI wa Taifa wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), John Heche, ametangaza kuwa Chadema imejipanga kumpeleka Ikulu Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa, kupitia katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 kufuatia hatua ya wananchi kuchoshwa na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya Kilombero mjini Arusha juzi   baada ya mapokezi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Heche aliwataka Watanzania kupuuza kampeni za kumchafua Dk Slaa, alizosema zimeanzishwa na kuratibiwa kwa  mamilioni ya fedha na watu kutoka ndani ya CCM wanaowatumia baadhi ya vijana wasaliti ndani ya Chadema.
Alisema tuhuma dhidi ya Dk Slaa kumiliki kadi ya chama tawala ni moja ya mikakati dhaifu inayotumiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye katika kumchafua kiongozi huyo.
Alisema hata hivyo mkakati huo haujafanikiwa wala hautafanikiwa kwa sababu umiliki wa kadi siyo hoja wala tatizo la Watanzania.
“Dk Slaa amewashinda CCM katika kiti cha ubunge Jimbo la Karatu kwa miaka 15 na alipojitokeza kuwani urais katika uchaguzi wa 2010, alitoa ushindani mkubwa ambao bado unawatia hofu CCM katika  uchaguzi ujao wa mwaka 2015 ndiyo maana wanawatumia wasaliti wachache kujaribu kumdhoofisha,” alisema Heche.
Hata hivyo, Chadema hakijatangaza rasmi iwapo Dk Slaa ndiye atakuwa mgombea urais kupitia chama hicho mwaka 2015.
Mwenyekiti huyo aliikumbusha CCM kuwa Dk Slaa wala Chadema siyo adui yao wala siyo sababu ya chama hicho kukosa haiba machoni mwa umma na kwamba adui wa CCM ni CCM yenyewe iliyoshindwa kutimiza mahitaji ya umma.
Alisema licha ya Tanzania kuwa nchi ya tatu duniani kwa uzalishaji wa dhahabu na rasilimali kadhaa, bado inaendelea kuwa Taifa maskini na ombaomba kutokana na viongozi wa CCM na
Serikali yake kuongoza kwa kujali masilahi binafsi, badala ya umma. Kuhusu suala la Dk Slaa kumiliki kadi ya CCM, Heche alisema kadi ya chama ni mali ya mwanachama ndiyo maana anakilipia na kwamba uanachama wa mtu hukoma pale anapokufa au kujiunga na chama kingine cha siasa.
Mwanancnhi

No comments: