Monday, December 24, 2012

ZAWADI YA X-MAS KWA RAY C, AISHA MADINDA, Q-CHILAH NA LANGA

Rehema Chalamila ‘Ray C’.

TANGU Januari hadi sasa Desemba kuna vitu vingi vilitokea katika ulimwengu wa burudani Bongo ambavyo naweza kuviandika wakati tukielekea ukingoni mwa mwaka 2012.
Langa Kileo.

Vyote naviweka kando, nawazawadia nafasi hii wasanii Rehema Chalamila ‘Ray C’, Aisha Mohamed Mbegu ‘Madinda’, Aboubakar Katwila ‘Q-Chilah’ na Langa Kileo.
Ni wasanii ambao mwaka huu walikiri na kuonesha mfano wa kuacha kutumia madawa ya kulevya. Ni idadi ndogo mno ukilinganisha na ile inayotajwa kila kukicha, wanaokimbizana Mitaa ya Kinondoni, Dar wakiwa wamechizika. Wakisumbuliwa na ‘alosto’. Wenyewe wanaita baga. 
Nakumbuka kuna msanii mmoja mkubwa aliulizwa na Salama Jabir kupitia kipindi cha Mkasi kama ni kweli anatumia madawa ya kulevya, akawa mbogo. Akasema hataki kuzungumzia masuala hayo ila aachwe aendelee ‘kuogelea’ akimaanisha kutumia madawa ya kulevya yaani unga na siyo bangi ambayo baadhi ya wasanii wameifanya kama mboga ya ugali.
Aisha Mohamed Mbegu ‘Madinda’.

Watajwa hapo juu, nawapa zawadi ya Krismasi kwa kuwapongeza kwa kuwa walijua wameanguka, wakakubali udhaifu wao na sasa ni wanaharakati wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya, kuanzia kwa wasanii wenzao hadi kwa jamii nzima.
Kupitia safu hii, miezi kadhaa iliyopita mwaka huu nilimzungumzia Ray C aliporejea Bongo akitokea nchini Kenya. Nakumbuka tulikubaliana tukutane Jumapili moja nyumbani kwa mama yake Bunju, Dar ili tujadili kuhusu kazi yake ya muziki lakini makubaliano hayakutimia kwa sababu muda ulipowadia simu yake haikuwa hewani wala nyumbani hakuwepo.
Yalisemwa maneno mengi kwa sababu ndicho kipindi alichoonekana ‘kudata’ lakini kama ujuavyo hujafa hujaumbika! Alijikubali, akajipenda, akakubali matibabu na sasa Mungu mkubwa.
Kama ilivyokuwa kwa Ray C, Langa naye alikiri kubobea kwenye unga lakini alipotazama nyuma akaacha na sasa anasaidia wenzake. Langa pokea zawadi yako ya pongezi kwa ajili ya Krismasi!

Aboubakar Katwila ‘Q-Chilah’.

Kwa upande wake Aisha Madinda alisifika kwa kukata nyonga jukwaani. Akaingia kwenye unga, maradhi yakamwandama na sasa anafundisha namna ya kuacha madawa ya kulevya pale Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Ni baada ya kukoswakoswa na kifo kwani unga ulikuwa ukimpeleka puta.
Ni juzi tu, Q-Chilah au Mtoto wa Magomeni ambaye ni legendari wa Bongo Fleva aliyewavutia vijana wengi kuimba wakiwemo akina Nasibu Abdul ‘Diamond’, naye alikiri kutumia unga kwa muda mrefu lakini unajua kitu kizuri alichokisema? Ana takribani miezi saba tangu alipoamua kuachana nao na anajiona wa tofauti akiipiga vita tabia hiyo hatarishi.
Marry Christmas!

Chanzo" GPL

No comments: