Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe, amewalipua Wazungu kuwa ni waporaji wakubwa wa rasilimali za Afrika.Pia ameitaja Uswisi moja kwa moja kwa moja kuwa inakumbatia sera ambazo zinasaidia uporaji wa rasilimali hizo kwa kuweka vivutio vya kutokulipa kodi na taratibu ngumu na zisizo wazi katika kufuatilia fedha zilizoporwa katika mataifa ya Afrika.
Alisema uporaji huo kwa kiasi kikubwa unaziumiza zaidi nchi nyingi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa njia ya ukwepaji kodi, rushwa na hila nyingine katika sekta ya uwekezaji.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema hayo wakati akihutubia mkutano wa masuala ya ushirikiano wa uchumi kati ya Ujerumani na nchi za Afrika.
Mkutano huo wa siku tatu mfululizo, kuanzia Desemba 9, mwaka huu, unafanyika mjini Berlin, nchini Ujerumani.
Zitto anatoa kauli hiyo wakati kukiwa na harakati kubwa nchini za kutaka Watanzania walioficha zaidi ya Dola bilioni 300 katika mabenki ya Uswisi wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kurejeshwa kwa fedha hizo nchini.
Miongoni mwa watu wanaodaiwa kuficha fedha hizo Uswisi ni pamoja na watumishi wa umma na viongozi waandamizi.
Katika mkutano wa jana, Zitto alisema kuwa nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikiporwa maliasili zake na baadhi ya kampuni za kimataifa kupitia ukwepaji kodi pindi zinapokuja kuwekeza barani humo.
Zitto alisema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mwaka 2012 katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (Unctad), jumla ya uwekezaji wote uliofanyika duniani kwa mwaka jana ni trilioni 1.5 (Dola moja ni sawa na Sh. 1,568) lakini kiasi cha fedha kilichotoroshwa kutoka nchi zinazoendelea kwa mwaka ni wastani wa Dola za Marekani trilioni 0.84 kati yake Dola trilioni 0.58 zilitoroshwa kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kibaya zidi Zitto alisema wakati kiasi cha Dola za Marekani bilioni 538 zinaibwa kutoka Afrika kwa nji za rushwa, ukwepaji wa kodi na mbinu za kutokulipa kodi, ni kiasi cha Dola za Marekani bilioni 80 tu kinaingizwa barani humo kama uwekezaji wa moja kwa moja na misaada.
“Kwa kila Dola moja inayokuja Afrika, Dola nyingine saba zinatoroshwa kutoka Afrika kupitia njia haramu! Hii haikubaliki,” alisema Zitto katika mkutano huo unaozungmzia pia jinsi kampuni zinavyowajibika kwa jamii kwa kurejesha kila wanachochuma.
Alishauri kuwa uporaji huo ni lazima uzungumziwe kama moja ya ajenda za ushirikiano wa maendeleo baina ya mataifa ya Afrika na yaliyoendelea.
Alisema kwa mujibu wa taarifa kuhusu uadilifu wa matumizi ya fedha duniani ya mwaka jana, kati ya mwaka 2000 hadi 2010, zaidi ya Shilingi trilioni 1,331.8 (Dola za Marekani bilioni 844) ziliporwa kwa mwaka kutoka nchi zinazoendelea kati yake ya fedha hizo, asilimia 69 zilichukuliwa kutoka nchi za Afrika.
Kwa mfano, Zitto aliuambia mkutano huo nchi kama Uswisi na nyinginezo zenye misamaha ya kodi, zinasaidia sera zake kufanikisha utoroshaji wa fedha kutoka mataifa masikini ya Afrika na pia zinaweka taratibu ngumu za uwazi juu ya fedha hizo hali aliyosema inasaidia kuongeza umasikini Afrika.
Alitaka mataifa rafiki kama Ujerumani kusaidia mataifa ya Afrika katika juhudi za kukataa uporaji unaofanywa na mataifa yenye sera kama za Uswisi.
Zitto aliuambia mkutano huo kwamba Tanzania inaongoza kupokea misaada kutoka nje baada ya Iraq na Afghanistan, lakini bado zaidi ya theluthi moja ya watu wake wanataabika katika umasikini.
“Hali ni hiyo hiyo katika nchi nyingi za Afrika. Mageuzi ya Ushirikiano wa Maendeleo ni yale ya kuwawezesha watu kuamua hatima yao wenyewe," alisema.
Huku akiitaka Ujerumani kuwa mdau na mshirika wa kusaidia mabadiliko ya kimahusiano ya uwekezaji ili mataifa ya Afrika yaamue kuhusu hatma yake yenyewe, alimnukuu hayati Mwalimu Julius Nyerere katika kitabu chake cha Uhuru na Maendeleo akisema:
“Mtu ajiendeleze mwenyewe akikua au akipata kipato cha kujitosheleza na kutunza familia yake. Atakuwa hajaendelea kama atapatiwa vitu hivi na mtu mwingine.”
CHANZO: NIPASHE
4 comments:
namungua mkono kadogo zitto lakini hili si geni kwani hajui yeye kwamba ufisadi hajaanza leo wala jana halafu kesi ya kima unampelekea nyani unadhani atakutetea wewe eti wazungu wanapora mali asili yetu kwani ni geni hili kila pembe ya dunia wanafanya hivyo na wao ndo wanajidai watetezi wetu na kutuwekea masharti na vyombo vyote vya haki wanavilinda wao kwa maslahi yao meaning huwezi kumpelekea sokowe kesi za nyani na kimma ni jamii mmoja.
wanaoiba na kupora na mafisadi wetu wa nchi wanakula nao sahani mmoja bwana dunia hii ni transit fanya wema uondoke thats all hakuna mtetezi wa mtu yeyote hapa ila mungu tu peke ndo mtetezi wa kweli na wa haki ndo maana hawawapendi wacha mungu ukiwa huna dini au hoe haee hujui dini yako basi ndo wanakupenda wao kwa sababu wata ku control
na bwana mdogo zitto kabwe wewe ni wa dini gani? unakaa bungeni wakati wa salaa ya ijumaa? hata kutete kwamba tupewe muda wa kusali ijumaa sijakusikia haata siku mmoja pale bungeni ni wa dini gani mwenzetu au rasta fara wenzetu wanapokuwa katika sehemu zao za kazi wanatetea dini yao pia au kuwa watiifu na dini yao wewe ni wa dini gani bwana mdogo tuambiye au hata kama hutaki kutuambia kumbuka mungu wako kuna siku utakuja kumuona.
ahsante wasiliasha mada ya uporaji may be one day kesi ya nyani na kimaa sokoo ataitetea kwa haki ha ha ha ha
".....na bwana mdogo zitto kabwe wewe ni wa dini gani? unakaa bungeni wakati wa salaa ya ijumaa? hata kutete kwamba tupewe muda wa kusali ijumaa sijakusikia haata siku mmoja pale bungeni ni wa dini gani mwenzetu au rasta fara wenzetu wanapokuwa katika sehemu zao za kazi wanatetea dini yao pia au kuwa watiifu na dini yao wewe ni wa dini gani bwana mdogo tuambiye au hata kama hutaki kutuambia kumbuka mungu wako kuna siku utakuja kumuona"
HEE..MAKUBWA HAYA TENA!..KWA HIYO ANONYMOUS HAPO JUU UNATAKA IJUMAA NAYO IWE NI SIKU YA KUSALI TU NA SIYO YA KUFANYA KAZI!..HIVI TUTAFIKA KWELI?..MAANA KUNA DINI KIBAO KATIKA ULIMWENGU HUU, KUNA WANAOSALI ALHAMISI,KUNA
WENGINE WANASALI JUMATATO..N.K, SASA MKUU SIKU HIZO ZOTE TUKIFANYA NI ZA KUPIGA MSWALA HAYO MAENDELEO YATAKUJA VIPI SASA?
nashangaa dini inaingia kwenye nini sasa hapa?
mtashanga sana dini inaingia kwenye nini hapa msishangaye na yenu yanakuendeeni mnapata chenu cha wenzenu midomo inakupayukeni na akili zinakuchemkeni wakiyasema hadharani, hata kama kuna dini kibao kuna ubaya gani walio na dini yao wasisimamiye dini yao wande kusali kwa vile jumapili mmepewa offu kwa nini basi tusilifunguwe bunge siku ya jumapili.
maendeleo gani hayo toka tupate uhuru maendeleo gani umeyaona zaidi ya ufisadi kwenda mbele na kuwaharibu watu akili zao especially watoto wadogo badala ya kuwapa elimu itakayo kuja kuwafaa mnawafanya vibaraka wenu maendeleo gani unayozungumzia.
maendeleo hayatakuja katika nchi yeyote ikiwa hakuna haki sawa kwa wananchi wake wote na zulumua ikizidi ndo nchi inazidi kudidimia na kuangamia.
eti mabkubwa haya bado hujayaona makubwa hamshangai kwa nini dini inaingizwa mtu mwenye akili yake ajiulize KWANINI UKITEULIWA UNAAPISHWA KWA KUSHIKA BIBILIA AU QURANA KWA NINI KAMA DINI HATAKIWI INGIZWE KWENYE SIASA KWA NINI, KWANI HAKUNA WASIO NA DINI KWA NINI IWE MNAAPISHWA KWA VITABU HIVI VITUKUFU VYA DINI ZENU KWA NINI.
watanzania wa hii leo sio tena bongo lala na mabumbubu wanachunguza kila kitu na walio na macho wataona na kusikia na kuchambua hoja bila matatizo yeyote kwa sababu ni wafikiri na watafakari sio watumwa wa kuburuzwa ovyoo kifikra mpo watoa madaa wenzangu.
kuweni wafikiri sio wafikiriwa na kuweni huru kuzichambua hoja sio domo kaya.
bwana mdogo zitto kabwe wewe ni wa dini gani? si lazia ujibu bwana mdogo lakini kumbuka kuna siku utamuona muumba wako na utamueleza wenzenu wanashika dini zenu nyinyi mnadanganywa na kasumba za uhuru wa bendera kwamba msichaganye dini na siasa jeulize kwa nini basi niwe nasika bibilia au quran katika kula kiapo nikishika nyazifa sherikalini au kwenye chama changu kwa nini
kazi kweli ipo mungu akusaidiyeni kufikiri
Post a Comment