CARDIFF, Uingereza
MAMA aliyempiga mwanaye wa miaka saba hadi kifo kwa kushindwa ‘kukariri kwa kichwa’ mistari ya Quran Tukufu amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Ilielezwa mahakamani kwamba baada ya kubaini kuwa kipigo hicho kimesababisha kifo cha mwanaye, mama huyo, Sara Ege (33) alichukua uamuzi wa kuuchoma mwili wake ili kuficha ushahidi.
Baada ya kusomewa hukumu hiyo, mama huyo alizimia kizimbani hivyo kulazimika kusaidiwa kwa kuondolewa katika kizimba cha mahakama hiyo, baada ya kuelezwa kwamba hatahusishwa kwenye msamaha wa aina yoyote hadi atakapotumika miaka 17 gerezani.
Mahakama hiyo ilielezwa kwamba mama huyo alimnyanyasa mwanaye “kama mbwa” wakati alipokuwa akihangaika angalau kukumbuka kwa kichwa mistari michache ya kitabu hicho kitukufu cha dini ya Kiislamu.
Ilielezwa kwamba aliendelea kumuadhibu kwa kumpiga kwa miezi mitatu mfululizo akimlazimisha kukariri mistari ya kitabu hicho, hadi alipodondoka akiwa chumbani kwake huku akiendelea kujaribu kutekeleza amri ya mama yake, kisha kuzimia na kufariki dunia.
Mama huyo alidaiwa kutumia mafuta maalumu kuuchoma moto mwili wa mwanaye huyo, ambapo watoa huduma za dharura awali waliamini kwamba aliuawa kwenye ajali ya moto iliyotokea katika nyumba ya familia huko nyumbani kwao, Welsh.
Uchunguzi wa awali wa mwili wa mtoto huyo ulibaini kwamba alifariki dunia kabla ya kutokea kwa moto huo na alikuwa na majeraha kadhaa ya ndani kwenye mwili wake ikiwemo kuvunjika mbavu, kuwa na mpasuko kwenue mfupa wa mkono na kuvunjika kidole.
Katika mapitio ya kesi hiyo yaliyochapishwa baada ya Ege kuhukumiwa kifungo hicho, mmoja wa wafanyakazi kwenye Shule ya Msingi Yaseen alieleza kwamba aliwahi kushuhudia matukio zaidi ya mawili ya mtoto huyo kufika shuleni akiwa na majeraha yanayoonyesha kuwa yalitokana na kipigo, lakini walihofia kutoa taarifa polisi.
Baadhi ya majirani zake walieleza kwamba motto Yaseen alikuwa akipata tabu kwa mateso nyumbani kwao, lakini hawakuwa na namna ya kumsaidia kwa haraka kutokana na tabia ya mama yake. Mahakama hiyo ilielezwa kuwa mama huyo, Ege ambaye ni mtaalamu wa Hesabu ambaye pia aliweza kupata nafasi ya pekee kutokana na uwezo wake wa kukariri mistari ya Quran Tukufu alipata tabu sana baada ya kuhangaika kutafuta mtoto kwa muda mrefu.
Mahakama hiyo ilielezwa kwamba kabla ya kuzaliwa kwa Yaseen, mama huyo alipata misukosuko ya uzazi na kwamba hiyo ilitokana na kutokuwapo uhusiano mzuri baina yake na mumewe ambaye alikuwa ni dereva wa taxi, pamoja na mama mkwe wake.
Pamoja na matatizo hayo, Ege alionekana kuwa mama aliyemjali sana mwanawe na aliendelea kuhakikisha kwamba anakua vyema.
Pamoja na matatizo hayo, Ege alionekana kuwa mama aliyemjali sana mwanawe na aliendelea kuhakikisha kwamba anakua vyema.
Hali ilianza kuwa mbaya baada ya wazazi hao kuwandikisha Yaseen katika shule maalumu kwa ajili ya kujifunza Quran, ambapo walitaka awe Hafiz, yaani kuwa na kumbukumbu kubwa kichwani kuhusu mistari ya kitabu hicho, wakitarajia kuwa hali hiyo itarejesha heshima kwenye afya.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment