Advertisements

Sunday, January 27, 2013

DCI Manumba apelekwa Afrika Kusini

Robert Manumba
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI),
 
NA BEATRICE SHAYO
Hatimaye Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, amepelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi.

DCI Manumba alilazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam Januari 15, mwaka huu baada ya kuugua kwa kile kinachoelezwa kuwa ni malaria kali na kusababisha figo kutofanya kazi.

Akizungumza na NIPASHE Jumamosi jana, msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Seso, alisema DCI Manumba alisafirishwa juzi kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi.

Alisema uamuzi wa kusafirishwa umekuja baada ya hali yake kuimarika na madaktari kuona ana uwezo kumudu kusafiri kwa ndege.

Hata hivyo, Senso hakuwa tayari kutaja Hospitali ambayo Manumba anakwenda kutibiwa "DC Manumba alihamishwa juzi kutoka Hospitali ya Aga Khan na kupelekwa Afrika Kusini baada ya hali yake kuimarika," alisema Senso.

Mkurugenzi huyo wa Makosa ya Jinai awali alilazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na baadaye alihamishiwa Aga khan na kulazwa katika chumba maalum cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU) baada ya hali yake kuwa mbaya.Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Aga Khan Dk. Jaffer Dharsee alithibitisha kuondoka kwa Manumba Hospitalini hapo .

"Ni kweli DCI Manumba amehamishwa hapa na kwenda Afrika Kusini, lakini hospitali gani anapopelekwa sifahamu," alisema Dk. Dhersee.

Hata hivyo, aliahidi kutoa majibu kamili ya Hospitali atakapolazwa baada ya kuandaa taarifa yake kwa umma.

No comments: