MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Bocco
Na Khadija Mngwai
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Bocco, anatarajia kupelekwa nchini India keshokutwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kifundo cha mguu wake wa kulia.Bocco alipata tatizo hilo wakati akiitumikia Kilimanjaro Stars katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Desemba, mwaka jana nchini Uganda.
Akizungumza na Championi Jumatano, Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, alisema uongozi umeamua kufanya hivyo kufuatia mguu huo kumsumbua mara kwa mara.
“Kikosi cha Azam kwa jumla kipo safi na hakuna majeruhi hata mmoja, wachezaji wote wanaendelea na mazoezi isipokuwa John Bocco ambaye inajulikana kuwa anaumwa tangu awali na uongozi umeamua kumpeleka India kufanyiwa uchunguzi wa mguu wake ili kuweza kugundua nini tatizo hasa.
“Kwa sasa tayari ameshaanza mazoezi mepesi na huwa tunamchezesha kidogokidogo na kumsimamisha ili kuweza kuona maendeleo yake kabla ya safari yake ya India, Januari nne,” alisema Mwankemwa.
Daktari huyo alisema utaratibu wote wa safari umeshakamilika na kinachosubiriwa ni siku ifike ili aweze kuondoka ambapo atasindikizwa na kiongozi mmoja wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment