ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 29, 2013

MALI, GHANA ZATINGA ROBO FAINALI AFCON 2013

Solomon Asante wa Ghana (kushoto) akimtoka Kourouma Fatokouma wa Niger wakati wa mechi yao ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyopigwa leo katika Uwanja wa Nelson Mandela, Afrika Kusini. Ghana wameshinda 3-0 na kufanikiwa kutinga Robo Fainali ambapo watakutana na Cape Verde. Mabao ya Ghana yamefungwa na Asamoah Gyan, Christian Atsu na John Boye.
Seydou Keita wa Mali (kulia) akiwania mpira na Jean Kasusula wa DRC wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mataifa Afrika uliopigwa katika Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban, Afrika Kusini. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1. Bao la DRC limewekwa kimiani na Dieumerci Mbokani wakati la Mali likifungwa na Mahamadou Samassa. Kwa matokeo hayo, Mali wamesonga mbele katika hatua ya Robo Fainali na watakutana na Afrika Kusini.

(PICHA NA MTN FOOTBALL)

No comments: