Advertisements

Wednesday, January 9, 2013

Mwandishi wa Redio Kwizera Issa Ngumba Ameuliwa Porini na Watu Wasiojulikana!!


Issa Ngumba.
Mwandishi wa habari wa Radio Kwizera anayefanyia kazi wilayani Kakonko mkoani Kigoma Bw. Issa Ngumba aliyepotea katika mazingita tata amekutwa amekufa na kunyofolewa sehemu zake za siri 
Taarifa kutoka Kigoma zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa mwili wa mwanahabari huyo umekutwa nje kidogo na mkoa wa Kigoma. 
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma RPC Kishai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi . 

Mbunge wa jimbo la Kigoma Zitto Kabwe pia amepata kuzungumza na mtandao huu na kudai kuwa ameguswa na kifo cha mtangazaji huyo na kutaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya kifo chake 
Pia Kabwe ameeleza jinsi ambavyo mwanahabari huyo alivyoweza kuifanya kazi yake kwa jamii ya Kigoma kwa ufanisi zaidi na kuwa wakati mwingine yeye kama mbunge alikuwa akizunguka na mwanahabari huyo katika jimbo lake. 
" Kweli nimeguswa sana na kifo cha kusikitisha cha mwanahabari huyo nilimfahamu vema kwa utendaji kazi wake ila nawapa pole sana waandishi wote nchini kwa msiba huu mkubwa .....na zaidi nitapata kueleza mengi mara baada ya uchunguzi" 
Taarifa za awali zilizotolewa na Jeshi la Polisi wilayani Kakonko baada ya kupotea kwa mwanahabari huyo zilisema kuwa Bw Ngumba alipotea tangu January 05 mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo alimuaga mke wake Bi. Rukia Yunus kuwa anakwendwa Muhange senta wilayani Kakonko na kwamba hajarudi nyumbani hadi sasa. 
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Muhange wanaendelea kumtafuta katika mapori ya kijiji hicho baada ya rafiki zake kueleza kuwa aliwaanga kuwa anakwenda kutafuta dawa msituni. 
Issa Ngumba. 
Aidha jeshi la polisi Wilayani Kibondo liliomba kampuni za mitandao ya simu anayotumia Bw Ngumba kusaidia kutambua simu zake zilipotumika kwa mara ya mwisho ili kurahisisha upatikanaji wake. Akizungumza kwa njia ya simu, Mke wa Bw Issa Ngumba, Bi Rukia Yunus amesema kuwa wananchi walio wengi ambao walikuwa wakimtafuta maporini wamerudi kijiji hapo baada ya kumkosa.

Maswali yaliyo jitokeza!!
1. Kawaida redio hiyo hutangaza taarifa/habari za aina gani?
2. Ngumba amekuwa akiandika habari/taarifa za aina gani?
3. Je, ni mwandishi mwololo au ana mtima wa nyundo?
... 4. Je, ni mtafiti/mchunguzi na mchambuzi (alikuwa na kipindi maalum redioni)?
5. Mahusiano yake na wenzake yalikuwa ya namna gani?
6. Mahusiano yake na wenye chombo yalikuwaje?
7. Mara ya mwisho aliandika habari zipi (zilihusu nini, nani na wapi)?
8. Anafahamika kwa kuandika nini kilichosisimua nywele za wengi?
9. Kazi yake iliyowahi kuibua mjadala miongoni mwa wenzake, mwajiri na wasomaji?
10. Alikuwa anapanga kufanya nini/kufuatilia nini (kile ambacho wenzake walifahamu)?
11. Alikuwa na uhusiano wowote na polisi (upi)?
12. Uhusiano wake na watawala wilayani ulikuwa wa aina gani?
13. Je, ni mwandishi aliyejua mambo mengi na ya ndani ya utawala wilayani?
14. Je, ni mwandishi aliyejua biashara za wazi na siri za "wakubwa?"
15. Mbali na kituo chake cha redio, alikuwa akipeleka wapi kazi zake (zipi)?
16. Uhusiano na mkewe ulikuwa wa aina gani (kwa mujibu wa watu wa karibu)?
17. Alikuwa na tabia gani (majivuno, ukarimu, wepesi/uzito wa kuelewa, ushabiki wa mambo (yapi); au alikuwa mpigania haki, mpenda kujielimisha na mtafutaji aliyetaka kuleta mabadiliko katika kazi/maisha/familia yake (vipi)?
18. Alikuwa na watoto (wangapi, wako wapi)?
Maswali haya nimempelekea pia mwandishi Kayanda aliyeko Kigoma. Ni muhimu tujue angalau haya machache.
CHANZO:DarSlam Productions

No comments: