
Kwa siku nzima jiji la Dar es Salaam lilitawaliwa na taarifa za wanamuziki kadhaa mashuhuri waliokimbia bendi zao na kwenda kujiunga na bendi nyingine ya Orchestra safari Sound, iliyokuwa ikijulikana kama OSS.
Kilichosimamisha mazungumzo ya wadau wa muziki na kuelekeza maoni yao juu ya tukio hilo, ni umahiri wa wanamuziki waliotajwa katika tukio hilo na hatima ya bendi walizozikimbia.
Kadhalika wapo waliokuwa wakikosa picha ya kujua hali itakavyokuwa kule OSS ambako kundi hilo linaelekea.
Kuhusu bendi zilizoangaliwa kwa jicho la huruma ni pamoja na Orchestra Mlimani Park, ambayo iliondokewa na wanamuziki takriban sita wakiwemo waimbaji wawili nguli Muhidin Gurumo na Hassan Bitchuka.
Si hao tu bali pia wapiga magitaa watatu, Kassim Rashid Kizunga aliyekuwa mpoga solo, Charles John Ngosha aliyekuwa akipiga ridhim na Ally Makunguru aliyekuwa mahiri kwa upapasaji wa gitaa la ridhim nao walikuwa mkiungoni mwa waliokuwemo safarini.
Kazi haikuishia hapo bali hata mcharaza dram hatari enzi zile Chipembele Saidi au Bob Chipe naye akawemo kundini.
Kama isingekuwa ujasiri wa wanamuziki wengune nguli kama Cosmas Chidumule, Fresh Jumbe Mkuu, Benno Villa Anthon Magari na wengine kadhaa basi huenda mwaka huo wa 1985 ungekuwa ndiyo mwisho wa historia ya bendi hiyo.
Kabla ya pigo hilo, Sikinde Sikinde ilishachapwa tena kibao cha uso pake bendi iliyokuwa ikimilikiwa na Shirika la Bima la Taifa NIC kuwanyakua wanamuziki wanne kutoka bendi hiyo, mwimbaji Shaaban Dede, Joseph Mulenga, Abdala Gama na Suleiman Mwanyiro waliokwenda kuiimartisha bendi hiyo na kuasisi mtindo wa Magnet Tingisha.
Waliokuwa wakiiangalia Safari Sound walipata kigugumizi juu ya wanamuziki hao wenye asili ya hapa Tanzania watakavyokwenda kushirikiana na wenzao kutoka Zaire sasa DRC.
Kabla ya hapo ilikiuwa si rahisi sana wanamuziki hawa kuwepo katika bendi moja hasa wale wanaounda safu ya uimbaji.
OSS tayari kulikuwa na wanamuziki kama Kabeya Badu, Skassy Kasambula, Tshibanda sony Wakabala, Kiliba Numbi Vikii, Akulyake Saleh au King Maluu, Mutombo Sozy Tomaa na wengine kadhaa.
KItendawili hicho kiliweza kuteguliwa baada ya kundi hilo lenye mchanganyiko wa pekee kuingia kwenye Studio na kurekodi nyimbo kadhaa huku zikiwachanganya wanamuziki hao wa makundi mawili.
Nyimbo za awali zilikuwa ni Shukurani kwa mjomba, Chatu Mkali, Pongezi kwa mama na Rehani ambazo zote zimepigwa kwa njia ya ushirikiano.
Katika vibao vyote hivyo imepatikana bahati ya wimbo mmoja tu ambao umewatenganisha wanamuziki hawa, kama ni makusudi au kwa kutojua.
Wimbo huo ulipewa jina la ‘Kusinzia kwenye matanga’ ambao ulitungwa na Kabeya Badu halafu ukaimbwa na waimbaji wote wenye asili ya DRC niliowataja hapo juu, lakini kwa uopande wa ala wakapiga Watanzania.
Ulikuwa ni wimbo uliotokewa kupendwa kama zile nyingine Salmada ulitungwa na Skassy au Sister Roboti, Kipanga na nyingine zilizokuwa zikitesa katika ukumbi wa Silent inn Mwenge jijini Dar es salaam.
Mada ya makala haya ni kuona jinsi wanamuziki wa dansi walivyoweza kufanya kazi katika mazingira yoyote na kufanikisha malengo yao kwani katika kipindi chote ambacho Ndekule ilikuwa na wanamuziki hao haikuwahi kufunikwa na bendi nyingine yoyote hapa nchini.
1 comment:
kuhama kwa akina shabani dede mwaka 84 haikuwa kitu kwa wana mlimani, na mwaka 85 walianza bitchuka na gurumo baadae wakafuata akina chidumule na wenzake, hapo hapo chidu,ule akaamua kurudisha majeshi sikinde na kutamba na wimbo wake neema, huku marehemu muharami said na akatoa kibao cha mv. mapenzi part 2.
sikinde kamwe haikutetereka mwaka 1986 nguvu mpya ikaongezeka akina beno villa anthony na fresh jumbe wakatia timu, mv.mapenzi ikaendelea kuchana mawimbi.
mmoja mmoja baadae walianza kurudi sikinde na hapo ikawa mwisho wa ndekule ochestra safari sound. kwa upande wa bima lee Abdalla Gama alikuwa wa kwanza kurudi sikinde hakukaa bima lee, Sleiman Mwanyiro pia kwa baadae alirudi sikinde, shaabani dede kama sikosei mpaka sasa yupo sikinde, wote watazunguka mwisho wntarudi sikindengoma ya ukae
Post a Comment