ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 26, 2013

UBALOZI WA WASHNGTON, DC WAMUAGA MHE. BALOZI MWANAIDI MAAJAR

Mkuu wa utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani mama Lily Munanka akiongea machache kumshukuru Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwananidi Maajar anayemaliza muda wake kwenye hafla futi iliyoandaliwa na Ubalozi huo maalum ya kumuaga Balozi huyo wakiwemo Maafisa wawili Brigedia Jenerali Maganga na Asia Dachi
Mhe. Maajar akimkaribisha Naibu Balozi wa Umoja wa Mataifa New York, Mhe, Ramadhani Mwinyi

Mkuu wa Utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani mama Lily Munanka katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Umoja wa Mataifa New York, Mhe. Ramadhani Muombwa Mwinyi
Mabalozi mbalimbali waliofika kwenye Hafla hiyo


Afisa Mindi Kasiga ndie aliyesherehesha hafla hiyo
Mhe. Mwanaidi Maajar katika picha ya pamoja na Mabalozi waliofika kwenye hafla hiyo
Charles Gray (kulia) Mmarekani anayetangaza Tanzania nchini Marekani na anayefuatilia sera za Mwalimu Nyerere akiongea jambo na Mabalozi waliofika kwenye hafla hiyi akiwemo mmoja wa wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Ujumbe kutoka California katika picha ya pamoja na Balozi
kwa picha zaidi bofya read more


 
 


Juu na chini Mhe. Mwanaidi Maajar akiwazawadia wafanyakazi aliofanyanao kazi kwa karibu

Brigedia Jenarali Maganga akiongea machache kutoa shukurani zake kwa zawadi na kuwaaga wafanyakai na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Brigedia Jenerali Maganga naye anarudi Tanzania baada ya kumaliza muda wake Ubalozini hapo kama mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada.
Kitengo kilichofanya kazi chini ya Brigedia Jenerali kikipata picha ya pamoja picha chini Brigedia Jenerali Maganga akiongea machache na kuwatambulisha
Juu na chini ni Mhe. Mwanaidi Maajar katika picha ya pamoja na wafanyakazi na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Mhe. Mwanaidi Maajar katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York Ramadhani Muombwa Mwinyi (watatu toka kusho) wafanyakazi na maafisa wa Ubalozi huo akiwemo mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York Hadji Khamis (kulia)



1 comment:

Anonymous said...

Nice pictures, great coverage. Kazi nzuri.