Wenzi wengi hulalamika kuwa wenzi wao wanapoanza kuonesha mabadiliko ya kitabia, inapotokea wakakwazana wakiwa ndani ya nyumba hata kwa jambo ambalo ni dogo, mmoja hujifanya kukasirika sana na kuondoka nyumbani bila kueleza anapokwenda, na anaporudi huwa amebadilika kabisa.
Uwezekano mkubwa ni kwamba mnapogombana, mwenzi wako anaweza kuwa anaitumia nafasi hiyo kikamilifu kwa kukutana na mpenzi wa nje kwa lengo la kujiliwaza.
*Kuanza kupendeza sana kimavazi anapotaka kutoka
Inaelezwa kuwa unapoona mwenzi wako akibadilika ghafla kitabia na kupenda kujiremba sana, kujipodoa na kuvaa nguo zinazomzidishia mvuto kuliko kawaida anapokuwa anataka kutoka, yawezekana anayafanya yote hayo kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wake mpya.
Unapaswa kuwa makini sana unapoona mabadiliko kama haya. Pia utamuona akianza kubadili aina ya mavazi aliyokuwa akipendelea kuyavaa, na zaidi atakuwa akipendelea mavazi yanayomfanya aonekane kijana.
*Kubadili marafiki ghafla
Unapogundua kuwa mwenzi wako amebadilisha marafiki na kuanza kushirikiana na watu wanaotia hofu, basi elewa kuna jambo nyuma ya pazia.
Unaweza kuona mwenzi wako akianza kuwa na uhusiano wa karibu na watu waliomzidi sana umri au ambao ni wadogo sana kuliko yeye.
Urafiki wa aina hii huwa ni kwa sababu kuna siri wanazofichiana au kuna mambo wanayoyafahamu wenyewe na hawapendi mtu mwingine afahamu.
*Kushindwa kupokea simu anapokuwa na wewe
Wengi wamekuwa wakilalamikia sana tabia hii, ambapo wenzi wao hushindwa kupokea simu wanapokuwa nao. Unakuta simu inaita halafu mwenzio anainuka na kwenda kupokelea nje. Hii ni dalili kuwa kuna mambo mabaya yanayozungumzwa ambayo mwenzi wako hapendi uyasikie.
Ukiuliza kwa nini hapokei simu akiwa na wewe atakupa visingizio vingi hata kudanganya juu ya mtu aliyekuwa anazungumza naye.
*Kupoteza msisimko wa kimapenzi anapokuwa nawe
Kwa mwenzi ambaye anakusaliti, moja kwa moja utaanza kuona akipoteza msisimko wa kimapenzi anapokuwa nawe, na si ajabu mkawa mnamaliza hata wiki nzima bila kuwa na hamu ya kukutana na wewe faragha. Unapomuomba huwa na kawaida ya kutoa visingizio vingi kama vile ‘Nimechoka kazini’, ‘Naumwa’, ‘Sijisikii vizuri’ na mengineyo ilimradi tu akwepe kukutana na wewe.
Kitaalamu kupoteza hisia hutokana na ukweli kuwa hisia zake huwa anakuwa amezihamishia kwa mtu mwingine
*Kuanza kukufundisha
staili mpya
Mwenzi anayekusaliti, huanza tabia ya kujisahau anapokuwa na wewe na kufikiri yuko na mpenzi wa nje. Inapotokea hivi, atajikuta akitaka kukufundisha staili mpya za kufanya tendo la ndoa, ambazo huwa anazitumia awapo na mpenzi wake wa nje.
Kwa lugha nyingine, huwa anaona kama umeishiwa mbinu za kumfurahisha hivyo kuanza kukufundisha kama yeye alivyofundishwa na mwizi wako.
*Kusema uongo
Dalili kubwa ya mtu anayekusaliti huwa ni kuongea uongo. Inaweza kuwa anakudanganya kwenye simu kuwa yuko mahali fulani na rafiki zake kumbe ni uongo, au mkikutana anakudanganya mambo mengi, uongo ambao muda mwingine huwa mgumu sana kuugundua.
Mpenzi mwaminifu huwa na tabia ya kuzungumza ukweli daima na hata ukimuuliza baada ya siku nyingi kupita kuhusu jambo alilowahi kukwambia, bado atakueleza kama alivyokueleza awali.
Mtu mwongo huwa na tabia ya kubadili maneno kila siku, kama jana alikuambia kitu fulani, ukimuuliza kesho atageuza maneno kabisa wakati anazungumzia jambo lilelile. Kuwa makini sana na mtu mwongo.
*Mikutano ya siri
Mpenzi anayekusaliti, atakuwa na tabia ya kukutana na watu kwa siri akitaka wewe usijue.
Utadanganywa juu ya muda ambao mwenzio alikuwa na mtu fulani, utaambiwa walikutana kwa bahati mbaya na walikuwa hawakupanga kukutana na walikuwa na maongezi ya kikazi na kikao cha harusi.
*Michezo au utani na watu wa jinsia tofauti
Unapoona mwenzio ameanza michezo na utani unaovuka mipaka na mtu wa jinsi tofauti, unapaswa kuwa makini kwani utani kama huo huishia kwa wahusika kuvunja amri ya sita. Pia inaweza kuwa ni utani uliopitiliza katika mazungumzo ya simu.
www.Globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment