ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 9, 2013

YANGA YAENDELEA KUJIFUA

Wachezaji wa Young Africans wakipasha misuli moto

Tmu ya Young Africans leo asubuhi imeendelea na mazoezi katika viwanja vya Fame Residence baada ya jana kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Denizlispor FC ya ligi daraja la kwanza Uturuki, mchezo ambao ulishia kwa Denizlispor FC kushinda kwa mabao 2-1, mechi liofanyika katika uwanja wa Selen football - Kamelya Complex Antalya.
Kocha Brandts ameendelea kukinoa kikosi chake na kufanyia marekebisho ya baadhi ya makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana ambao hata hivyo Yanga iliutawala kwa kipindi chote cha mchezo lakini maamuzi ya mwamuzi kipindi cha pili yaliinyima Young Africans ushindi.
Denizlispor FC timu ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya uturki mwaka juzi, inapigania kurudi tena katika Ligi kuuya Uturuki, jana ilishindwa kutamba kabisa mebele ya Young Africans ambayo iliweza kucheza soka safi na la kuvutia mda wote wa mchezo.
Brandts amemtupia lawama mwamuzi wa mchezo jana, kwamba maamuzi yake ndio yalipelekea timu yake kupoteza mchezo huo, kwani vijana wake waliweza kucheza vizuri kuanzia nafasi ya ulinzi mpaka ushambuliaji hali iliyowashangaza waturuki hao.

Tazama goli la kwanza mshambuliaji wao aliunawa mpira kabla ya kufunga na bado mwamuzi akalikubali bao alilofunga, bao la pili Nadri Cannavaro alichezwa mazdhambi mshika kibendera akanyanyua kuwa ni faulo lakini cha ajabu mwamuzi aliamuru ipigwe penati, kiukweli mwamuzi alichangia kutufanya tupoteze mchezo huo alisema 'Brandts'

Wachezaji wanaendelea na mazoezi mpaka siku ya jumamosi ambayo itakua ni siku ya mwisho kabla ya siku ya jumapili kuanza safari ya kurudi nchini Tanzania tayari kabisa kwa mbio za kuuchukua Uibingwa wa Ligi ya Kuu ya Vodacom 2013. 


Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezin leo asubuhi katika viwanja vya Fame Residence football


Young Africans imeendelea na mazoezi yake leo asubuhi katika viwanja vya Fame Residence Football ambapo imekuwa ikifanya mazoezi tangu kuwasili katika mjii wa Antalya.

Kabange Twite, Haruna Niyonzima & Mbuyu Twite

No comments: