ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 18, 2013

Binti augua Ugonjwa wa ajabu

FLORIDA, Marekani
HAKIKA hujafa haujaumbika, msemo huu unaweza kuufananisha na tukio lililomsibu mwadada Amanda Gryce kutoka kule nchini Marekani baada ya kukumbwa na ugonjwa ajabu.
Wengi wanaweza wakasema kwamba anapata  raha, lakini sio kweli kwani ugonjwa huu unamtokea sehemu yoyote ambapo haustahili kumtokea mtu wa kawaida hali ambayo kwa mujibu wake inamsababishia  karaha.    
Inafahamika kwamba kuishi maisha ya kupenda ngono kupita kiasi kwa wengi wetu ni maisha mabaya na yasiyofaa, lakini kwa Amanda Gryce si jambo la ajabu.
Binti huyu mwenye umri wa miaka 22 anasema, maisha yake yameharibiwa na mfumo wa homoni zake za mwili ambapo anaweza kufikia mshindo mara kwa mara anaposikia sauti za aina fulani.
Anasema sauti ya muziki, magari yanapotembea, treni na hata milio ya simu ni kati ya vitu vinavyomfanya kufikia hali hiyo mara kwa mara na kusababisha ashindwe kuwa huru katika maisha yake.
Hiyo inamtokea mara kwa mara iwapo anakuwa na marafiki zake na hata anapokuwa kazini kwake kama mkusanyaji wa mauzo kwenye duka la bidhaa za watoto huko Florida nchini Marekani.
Tatizo hilo linalomkumba Amanda ni nadra sana kutokea katika mwili wa binadamu hasa wanawake. Tatizo hilo liitwalo Persistent Sexual Arousal Syndrome (mwili kuendeleza masuala ya usisimuaji) au PSAS limesababisha kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Kwa mujibu wa Amanda anasema tatizo hili alianza kukumbana nalo alipokuwa na umri wa miaka minane tu, na sasa limekuwa tatizo sugu kwake.
Ingawa tatizo hili la PSAS ni nadra kutokea, inaweza kuwa na madhara makubwa kwa watu wachache ambao wanakabiliwa na hali hii.
Mwaka 2012, Gretchen Molannen 39, aliyekuwa akiishi Florida nchini Marekani, aliamua kujiua baada ya kuishi na tatizo hilo kwa miaka 16.
Tatizo hili limekuwa gumu pia kwa Amanda ambaye naye anaishi katika mji huohuo wa Florida, lakini binti huyu yeye anasema mara nyingine amekuwa akiamua kujichua hata mara 15 kwa siku moja ili kuweza kupata unafuu.
Anasema, “Sipati raha yoyote  unaweza kusema kuwa yamekuwa ni mateso. Hali hii inakuwa inaongoza maisha yako ya kila siku na ni kama kuishi katika ndoto.
“Ninafika mshindo mara 50 kwa siku na hii ni mara tano au kumi kila baada ya saa moja  hali hii inaniaibisha sana kwani inatokea nikiwa na marafiki zangu au nikitoka katika matembezi na inaniaibisha sana,’’ alisema.
“Hali hii inaniua mimi ndani kwa ndani. Inanibidi kuwa na tabasamu mara kwa mara usoni mwangu kana kwamba sina tatizo lolote.
“Watu wenye tatizo la kufikia mshindo mara kwa mara wanatakiwa kuwa na fikra nzuri kila wakati, lakini nakutana na hali hii kwa muda mrefu sasa na ninaishi kwa woga na aibu.”
Alifafanua: “Katika fikra zangu nikiwa mdogo, nilikuwa nafikiria kujiua, lakini nilijihakikishia kwamba siwezi kufikia hatua hiyo na kitu kama hicho hakiwezi kuja kunitokea.”
Amanda alianza kukutana na mateso hayo alipofikisha umri wa miaka nane tu, na alipofika umri wa miaka 13 alianza kupata hisia kali wakati akiwa ameketi darasani wakati wa masomo, hivyo ndivyo alivyoanza.
Lakini, kwa kuwa alikulia katika dini ya Kikatoliki na kufundishwa katika mafunzo maalumu ya ‘Sunday School’ kuwa mawazo ya ngono na kujichua  ni dhambi, alikuwa akishindwa kumwambia mtu yeyote kuhusiana na hali yake.
Kilio cha kuomba msaada
Hali hiyo ilizidi kupamba moto kwa Amanda kwani alianza kupata mawazo ya kujiua na kuna wakati alijaribu kutoroka katika familia.
Anasema, “Nikiwa kama mtoto, sikuwa na wazo nini nifanye kuhusiana na hali iliyokuwa imenitokea kwa ghafla, nilifikiri kwamba nilikuwa tu na mhemko wa ngono. Nilianza kujichua ili kupunguza makali, nilihisi hatia kila wakati nilipofanya hivyo.”
Ilikuwa ni kati ya mwaka 2008 aliposikia kuhusu PSAS na alipojaribu kusikiliza katika redio alianza kutafuta madaktari mbalimbali kwa ajili ya msaada.
Amanda alianza kwa kuwatembelea madaktari wanne. Aligundua kwamba hakuna aliyewahi kusikia hali hiyo.
Tangu wakati huo aliamua kuendelea na maisha yake na alipotimiza umri wa miaka 20 na baada ya kupoteza bikira yake, alifikiria kuwa ngono inaweza kusababisha hali yake kuwa mbaya zaidi.
Lakini pia alifikiria kuwa asingeweza kuwa na uhusiano thabiti kwa sababu aliona wanaume wanaweza kuchukulia hali yake kuwa kigezo au kutishiwa mara kwa mara.
Anasema “Baada ya kupoteza ubikira wangu mimi niliachwa na nilipata hisia za kuaibika. Haikunifanya mimi nijisikie vizuri. Mwanamume niliyekuwa naye awali alionyesha ushirikiano kwangu, lakini baadaye aliitumia hali yangu kujiridhisha yeye kimapenzi mara kwa mara.
“Nilikuwa na wanaume kadhaa awali lakini wamekuwa na ugumu kwa kila mmoja, kuna wanaume niliowahi kuwa nao ambao walijitahidi hata kunitishia uhai wangu.
“Nashukuru nimepata ujasiri wa kuiambia familia yangu na wao wote wamenielewa na kuniunga mkono katika hali yangu hii ya majonzi.”
Alidokeza: “Ninakutana na watu mbalimbali ambao wamekuwa wakinipa wakati mgumu, na kuna wengine wanaosema kuwa mimi nimejitakia hali hii na kwamba ninapenda ngono.
“Ninajipa moyo kwamba ipo siku, watu watapata ufafanuzi juu ya hali hii na hadithi yangu itawasaidia watu wengine hapo mbeleni kuweza kupata msaada.”
Tatizo la Amanda pia limekuwa likiwatokea baadhi ya wanaume na wengi wao wamejikuta wakiishia kubaka na hata kufanya vitendo vya aibu kwenye mikusanyiko ya watu, huku baadhi yao wakijichua mara nyingi kwa siku.
Herieth Makwetta  wa Mwananchi kwa msaada wa mtandao.


No comments: