Saturday, February 2, 2013

BINTI WA MIAKA 13 ATIWA MBARONI KWA KUFANYIWA KITCHEN PARTY DAR

Binti huyo (kushoto) akiwa chini ya ulinzi wa polisi akitolewa ndani na kuingizwa kwenye gari
Akina mama walikokuwa katika sherehe hiyo wakitahamaki baada ya kachero wa polisi kujitambulisha
akiingizwa kwenye gari ambapo alipelekwa Kituo cha Polisi, Stakishari kwa mahojiano zaidi.
Hakuna lugha nyepesi unayoweza kuzungumza zaidi ya kusema haya ni maajabu ya mwaka 2013, kwani familia ya Masoud Kassim wa Karakata. Ukonga Dar imejikuta ikiingia kwenye mgogoro wa kisheria baada ya kuamua kumfanyia ‘kitchen party’  mtoto wao wa miaka 13 aitwaye Rafia Masoud, tayari kwa ndoa.
Tukio hilo la kusikitisha na kuhuzunisha limetokea Jumatano ya wiki iliyopita ambapo mtandao huu ulikuta Rafia akiwa katika sherehe hizo huku ndoa yake ikitarajiwa kufungwa leo Februari 2.
Habari picha na Haruni Sanchawa wa GPL

1 comment:

  1. WASHITAKIN FAMILIA ZOTE MBILI WANAPOTEZA UTU NA UTOTO WA MTOTO KIPI KIKUBWA KWENDA KUMUOZA MTOTO . LOH LAANA ZA TAMAA TU ,WATANZANIA MKISIKIA MKIONA TOEN TAARIFA ZA WATU KAMA HAOAAA

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake