Saturday, February 2, 2013

RAIS KIKWETE APATA MAPOKEZI MAKUBWA KIGOMA

 
Kikundi cha Ngoma cha Wakinamama wa Kigoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete. 
 
Ndege ya Rais Kikwete ikiwasili Kigoma leo tayari kwa sherehe za miaka 36 ya CCM zitakazo fanyika kesho Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.  
Rais Kikwete akiteremka kwenye ndege leo katika uwanja wa ndege wa Kigoma tayari kwa sherehe za miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.  
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mjumbe wa NEC mkoa wa Kigoma Kilumbe Ng'enda mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Kigoma leo tayari kwa sherehe za kuzaliwa kwa CCM.
Mwenyekiti wa CCM akisalimiana na wananchi wa Kigoma waliokuja kwa wingi kumpokea , Mwenyekiti yupo Kigoma kwa ajili ya sherehe za miaka 36 ya CCM. 
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ndio Mwenyekiti wa CCM,akiwa pamoja na Nape Nnauye Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi kwenye uwanja wa ndege Kigoma. 
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza mtangazaji wa Radio Uhuru ,Stephen Mhina ambaye alitaka kujua pamoja na maendeleo yote yaliofanyika Kigoma, Mheshimiwa rais alimjibu kuwa "tunatimiza wajibu" 

Picha zote na Adam H. Mzee

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake