Hamis Kiiza (kushoto) akishangilia bao la kusawazisha ibwa Sugar, kulia ni Jerseon Tegete (picha na Mahmoud Zubery)
Young Africans imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar kutoka Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika leo jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo wa leo Young Africans imeshindwa kuondoka na ushindi kutokana na washambuliaji kushindwa kutumia nafasi nyingi za wazi hali iliyopelekea mchezo kuwa mgumu kwa kipindi chote cha mchezo.
Didier Kavumbagu na Jerson Tegete walikosa nafasi za mabao ya wazi zaidi ya tano katika kipindi cha kwanza, kwani umahiri wa mlinda mlango Sharrif Cassilas wa mtibwa uliweza kuwafanya waonekane bora muda wote wa mchezo.
Dakika ya 45, Shaban Kisiga aliipatia Mtibwa Sugar bao la kwanza kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Said Mkopi na mpira huo kumkuta mfungaji akiwa peke yake na kuukwamisha mpira kwa kichwa.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 1 Mtibwa Sugar.
Kipindi cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mbadiliko ambapo Said Bahunuzi, Hamis Kiiza na Nurdin Bakari waliingia kuchukua nafasi za Frank Domayo, Didier Kavumbagu na Athumani Idd.
Mbadiliko hayo yaliongeza uwezo wa kumiliki mpira kwa timu ya Young Africans kwani eneo la kiungo walilitawala vizuri hali iliyoplelekea kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Mtibwa Sugar lakini umakini wa washambuliaji bado ulikua ni tatizo.
Hamis Kiiza aliipatia Young Africans bao la kusawazisha dakika ya 86 akimaliza shuti kali lilopigwa na Said Bahanuzi kutoka upande wa kulia na kumkuta Kiiza aliyeukwamisha mpira huo wavuni na kuwa bao la kusawazisha.
Young Africans ilikosa tena mabao ya wazi dakika za lala salama kupitia kwa washambuliaji wake Tegete, Msuva, Kiiza na Bahanuzi ambao walikosa mabao hayo hali iliyopelekea wapenzi na wanachama wa Young Africans kukosa raha kutokana na nafasi hizo.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 1- 1 Mtibwa Sugar.
Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kikosi chake hakikucheza vizuri katika mchezo wa leo, wachezaji walipata nafasi nyingi za wazi lakini hawakuwa makini hali hiyo ndio iliyopelekea mchezo kuisha sare ya mabao 1-1.
Young Africans: 1.Ally Mustafa 'Barthez', 2.Mbuyu Twite, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athumani Idd/Nurdin Bakari, 7.Saimon Msuva, 8.Frank Domayo/Said Bahanunzi, 9.Didier Kavumbagu/Hamis Kiiza, 10.Jerson Tegete, 11.Haruna Niyonzima
Mtibwa Sugar: 1.Hussein Sharrif, 2.Said Mkopi,3.Issa Rashid, 4.Rajab Mihamed, 5.Salum Sued, 6.Shaban Nditi, 7.Vicent Barnabas, 8.Rashid Gumbo, 9.Hussein Javu, 10.Shaban Kisiga, 11.Ally Mohamed
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake