Brigedia Jenerali Maganga na mdhamini wa pendo lake, Love Maganga wameagwa rasmi na Watanzania wa DMV Jumamosi Feb 16, 2013 kwenye ukumbi uliopo College Park, Maryland, nchini Marekani. Brigedi Jenerali Emmanuel Maganga ni Mwambata wa kwanza wa Jeshi kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada anayemaliza muda wake na anatarajiwa kurudi nyumbani muda wote kuanzia hivi sasa.
Kutoka kushoto ni Brigedia Jenerali na Mke wake na Mr & Mrs Sichele waliokuja tokea North Carolina
Brigedia Jenerali Maganga na mkewe akiwa na Mrs Sichele (kushoto) wakijiandaa kuingia ukumbini
Brigedia Jenerali na mkewe wakiongea machache kuwashukuru wanaDMV kwa kuwaandalia sherehe ya kuwaaga.
Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar na Mumewe Bwn. Shariff Maajar wakijumuika pamoja na Watanzania wengine wa DMV kwenye sherehe ya kumuaga Brigedia Jenerali Maganga na mkewe (hawapo pichani) iliyofanyika Jumamosi Feb 16, 2013, College, Park, Maryland, nchini Marekani.
Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar akishuka kwenye gari lililomleta huku akilakiwa na Rais wa Jumuiya ya Tanzania DMV, Idd Sandaly.
kutoka kushoto ni Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Idd Sandaly, Mume wa Mhe. Balozi, Bwn. Shariff Maajar, Mhe. Balozi Mwanaiidi Maajar na Afisa Ubalozi Dr.Switebert Mkama wakimsikindikiza Mhe. Balozi kuingia ukumbini kwenye sherehe ya kumuaga Brigedia Jenerali Maganga.
Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar katika picha ya pamoja na Afisa Habari Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga
Brigedia Jenerali Maganga na Mkewe Love Maganga wakikata keki na kulishana kwa tabamu la kukata na shoka kama picha za chini zinavyojieleza.
kwa picha zaidi bofya read more
2 comments:
Tamia na Bahati mmependeza,mmmwahh!
shughuli ya kumuaga General Maganga ilipendeza sana ukilinganisha ya kumuaga balozi kule kwenye ukumbi wa Martin? ilikua mbaya sijawahi kuona mpangilio mbaya kama ule. pongezi zimfikie mwaandaaji maalumu Mr Mea
Post a Comment