
Wananchi waliofika kushuhudia ajali ya jengo la ghorofa nne lililoporomoka jana katika eneo la Mpakani B kata ya Kijitonyama.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:45 jioni baada ya nguzo za jengo hilo kutitia na kupelekea kuporomoka na hatimaye kusababisha kifo cha mtoto aliyetambulika kwa jina la Joha Jeremia.
Juhudi za kuokoa zilifanywa na kikosi cha zimamoto ambao walifanikiwa kumwokoa mfanyakazi wa nyumba hiyo aliyetambulika kwa jina la Clementina Kipanjula (19).
Mwenyekiti wa mtaa wa Mpakani B kata ya Kijitonyama Barbo Kalinga aliliambia NIPASHE kuwa ghorofa hilo lina zaidi ya miaka 20 na mmiliki wake anaitwa Charles Lukumai ambaye alishafariki miaka mingi iliyopita.
Alisema katika ghorofa hilo kulikuwa na familia yenye mama na watoto wawili pamoja na mfanyakazi wa ndani waliokuwa wanaishi.
Omary Athumani ambaye ni mlinzi wa ghorofa hilo alisema alisikia mlio wa kukatika kwa kitu lakini hakujua ni kitu gani, na ghafla akaona ghorofa linadondoka.
Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, hawakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment