Tuesday, February 5, 2013

HAPA NA PALE NI KHERI KUSIKIA NA IWE RAHISI KUSIMULIA LAKINI USIOMBE YA KUKUTE BARUA KUTOKA KWA PAPII KOCHA HADI IKULU KWA RAIS

BARUA YA PAPII KOCHA KWA RAIS JAKAYA KIKWETE... KWA WALE AMBAO HAMJAISOMA HÍI HAPA.

MF/NA: 836'04
Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam


Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania

YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga. Kwa heshma na
taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya KIMUNGU ulionayo dhidi ya binadamu
wenzako pamoja na mamlaka uliyokabidhiwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa Rais. Nakuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais, kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani,niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.
Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo, na ukweli kutoka moyoni sikufanya kosa hilo. Si mimi, baba yangu Nguza wala ndugu yangu yeyote aliyefanya kitendo kile.
Lakini wenye mamlaka wakatuona tuna hatia na kuamua kuteketeza kizazi chetu gerezani.

Natamani kiama ifike ili mwenyezi Mungu aweke wazi ukweli wote uliojificha nyuma ya pazia. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako
mitukufu Mh. Rais Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi. Lakini pia sisi ni binadamu wenye nafsi na miili kama wengine.
Waliotumia mamlaka yao kutuweka gerezani nao ni binadamu pia, wenye miili na nafsi. Ipo siku nafsi zetu zitapaswa kutoa hesabu ya tuliyoyafanya hapa duniani. wakati huo miili yetu tunayoitumia kunyanyasa wanyonge itakuwa imeoza mavumbini. Natumaini kauli yako ya mwisho
ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu. 

Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.

Mungu akubariki.
Wako mtiifu
Mfungwa NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)

5 comments:

  1. Nimependa barua yake,i hope rais wetu atampa msamaha,ukiangalia kwa undani zaidi inaonekan wamepandikiziwa,haiwezekani baba na vijana wake wakawa na kamchezo ka kuwa...watoto wadogo huku wakibadilishana,mimi binafsi siamini,hivi hakuna DNA bongo?hicho ndio mwisho wa matatizo,bila hivyo watu wataonewa sanaaa,wangefanya DNA kama wameingiliwa na hao watu pamoja na lie dectector!!!kwkweli ni ngumu sana,inatia huruma.Ila katika hii barua huyu Papii Kocha angeandika ni kosa gani alilofungiwa kwasababu inaonekana kafungwa anaomba msamaha but msamaha wa nini?kwa watu wasiojua au kiprofesheno zaidi na kimsamaha zaidi angesema ni kwa nini alifungwa(ingawa hakuna anaejua ukweli).ni hayo tu,Rais wetu tunajua una wafungwa wengi sana wanaotaka huruma yako na msamaha but liangalie na hili.Asante sana.

    ReplyDelete
  2. Kwako Mtukufu Rais wetu wa Tanzania J. K. Ni kweli kabisa kama Barua ya huyu Kijana jinsi alivyojieleza. Kila Binadamu anahitaji Kusamehewa ili na wewe pia Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema aje akusamehe Dhambi zako. Mbona Kina Elizabeth Michael (LULU) Wametolewa kwa Dhamana? Huyo Papii kama alivyokuomba ni kama Mwanao Mheshimiwa Rais wetu. Adhabu waliyokwisha itumikia ni imeshakuwa kwa Miaka mingi. Siwafahamu Papii na Baba yake ila nikiwa kama Mwanadamu inasikitusha. Mungu akauguse Moyo wake ili uweze kusikia HURUMA. Aksante. Mtanzania mwenzango.

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kabisa waliyoyasema wenzangu hapo juu mheshimiwa rais nakuomba na tunakuomba sisi watanzania wote barua ya papii kwa niaba yake na baba yake kwa heshima yako ukiwa kama raia na rais wetu wa tanzania pokea msamahaa huu .. asante.

    ReplyDelete
  4. Ndugu zetu Watanzania, Mliokuwa Wapenzi na Mashabiki wa Familia ya Nguza na Vijana wake. Unganeni ikiwezekana hata Muandamane hadi Ikulu kwenye Ofisi ya Mtukufu Raisi Jakaya Mrisho Kikwete kumuombea MSAMAHA Kijana na Baba yake. Kwa kweli Kiubinadamu Inauma Saana. Kama Mjumbe uliyesema kuwa Wafungwa ni Wengi, lakini kama mtu/watu wanaojitokeza kuomba na kuhurumuwa. Tunakuomba Rais wetu uliangalie swala hili Kiubinadamu na Kulifikiria. Biblia inasema JIFUNZE KUSAMEHE ILI NAWEWE USAMEHEWE. Sifahamuvkhsu Kuruhani Inavyosema kuhusu Kusamehe. Kweli mimi ni Mtanzania niliyeguswa na Kusikia Huruma sana kwa Mahakama kuwafunga Kifungo cha Maisha. Kijana barua yake Inasikitisha mnoo kwamba Ingekuwa ana uwezo wa Kiama Kifike iki Ukweli Ujionyeshe nadhani Rais wetu ungejisikia huruma ambayo sijui Ungeibadilishaje wakati wamekwisha kukitimikia Kifungo kwa Miaka Mingi hadi sasa.

    Mwenyezi Mungu akujalie Roho ya Imani ili ukalifikirie Ombi hili. Mbona Watanzania wengi wanaofanya Vitendo vya Kinyama vya MAUAJI akini Kesi zao Rais wetu unazijua na huwachukulii Hatua yoyote. Kesi zao zinazimwa Chini kwa Chini tuu!! Samehe ili nawe Usamehewe kwa yote Mabaya uliyoyatenda katika dunia hii.

    Aksanteni wote mlioguswa na Ombi la Kijana mdogo PAPII.

    ReplyDelete
  5. Nimeguswa sana na barua na ombi la Kijana mdogo Papii. Kama Mtanzania wenzangu, naomba Mheshimiwa Rais aliangalie na kuguswa jamaaani. Inatia huruma sana wanyonge wanapokosa pa kukimbilia. Siwafahamu lakini nakuomba Rais wetu uliangalie na kuguswa pia.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake