ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 28, 2013

Hatuna mpango wa kuwasaidia waliofeli kidato cha lV-Mulugo

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema wizara haina mpango wowote kwa sasa kuhusiana na wanafunzi waliofeli kidato cha nne mpaka pale Tume itakapomaliza kufanya kazi yake ndipo itaamua nini cha kufanya.
Mulugo aliliambia NIPASHE kuwa wizara inasubiri Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, imalize kufanya kazi yake, ndipo itatoa uamuzi nini kifanyike juu ya wanafunzi hao.
“Kwa sasa siwezi nikasema chochote kwani tume imeundwa ili kulifanyia kazi jambo hilo, hivyo tunasubiri wamalize kufanya kazi yao ndipo tutatoa kauli ya nini kifanye juu ya wanafunzi walio feli kama ni kurudia tena mtihani au la,” alisema Mulugo.
Alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa wizara yake inazungumziaje juu ya mpango wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu kuandaa mafunzo ya kozi ya muda mfupi kwa vijana wote waliofeli mkoani humo ili kuwapima kama wapo wanaaoweza kusaidiwa kuendelea na elimu ya cheti.
Msambatavangu alitoa uamuzi huo baada ya makubaliano yake na baadhi ya vyuo vikuu kama Chuo Kikuu cha Tumaini (IUCO) na Chuo kikuu cha Ruaha (Ruco) na kukubaliana kutoa mafunzo hayo yatakayo anza Machi mwaka huu. 
Mulogo alisema kuwa ni wazo lenye mpango mzuri wa kuwasaidia vijana wengi ambao ni kama wamekumbwa na tatizo kwa sasa, hivyo anacho kifanya Mwenyekiti huyo hakina madhara yoyote  na anafanya kama raia mwema aliyeguswa na matokeo hayo
CHANZO: NIPASHE

3 comments:

Anonymous said...

Wajameni watoto wa hawa kina bwana wakubwa wapo Uganda na Kenya wanasoma shule za private ndiyo maana wanatoa majibu yoyote wanayojisikia na hakuna wanalojali. Enzi zetu sisi mzazi wangu alikuwa Waziri enzi za Nyerere hadi Mkapa na tulikuwa wengi wetu watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule za kawaida hapo nchini na wazazi wetu walitusikiliza malalamiko yetu na kuyafuatilia kwa ukaribu. Hembu tujiulize mtoto gani wa waziri RC DG wa kampuni sasa hivi anasoma shule kama Muhimbili oysterbay Mbuyuni au sekondari kama Ndada, Kilakala, Jangwani au Zanaki????? HAKUNA SO UNATEGEMEA HAWA VIONGOZI KUJALI ELIMU YA WALALA HOI??? THIS IS AN ISSUE. NA SYSTEM HAIQUESTION KUWA HAWA WATU WANAPATA WAPI PESA ZA KUWASOMESHA WATOTO WAO HUKO NJE PAYING THOUSANDS OF DOLLARS? ENZI ZA BABA WA TAIFA KULIKUWA NA INTELLIGENCE YA HALI YA JUU KAMA SI KWA SCHOLARSHIP ZA KISOCIALIST CHINA URUSI BULGARIA BASI UTAITWA WITHIN 24 HRS UJIELEZE HOW YOU PAY YOUR KIDS SCHOOL FEES NJE NA ANAJUA MSHAHARA WAKO. THAT HOW IT WAS THEN. KILA KIONGOZI ANA DECLARE HIS OR HER WORTH NA OLE WAKO UDANGANYE, MZEE WANGU NAKUMBUKA IKIFIKA WAKATI HUU ANAKUSANYA BANK STATEMENT ZAKE ZOTE NA ZA MKEWE HATI ZA MASHAMBA HATA YA URITHI, DOCUMENT ZA GARI NA KILA KITU ANAJAZA HIYO FOMU WAKATI HUO TUME YA KUCHUNGUZA TABIA ZA VIONGOZI IKIONGOZWA NA MAREHEMU MZEE KITUNDU, HAKUNA KUPENYA!!!! Sasa hivi intelligence IMEKUFA BONGO!!!!!!!!!!!!!!!! Mabomu yanalipuka baada ya miaka kadhaa ya ufisadi, CAMON PEOPLE WATOTO WETU SI WAJINGA KIASI HIKI CHA KUFELI MITIHANI SERIKALI INATAKIWA IANGALIE MFUMO WA ELIMU NA AFYA. WALIMU NA WATIBABU NI WATU MUHIMU NA LAZIMA WAWE COMPASATED FAIRLY, BADALA YA KUFIKIRIA KUONGEZA POSHO ZA WAO KUKALIA VITI BUNGENI WAWAFIKIRIE WALIMU NA KIPATO KIKIWA KIZURI BASI WATU WENGI WATACHUKUA HII FANI YA UALIMU NA SUALA LA UKOSAJI WA WALIMU HASA WA MASOMO YA SAYANSI UTAPUNGUA. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Anonymous said...

Deputy Minister of Education and Vocational Training Philip Mulugo, said the ministry does not plan to present any relation with students ...

Anonymous said...

Ingawa alisema wazo hilo halijapitishwa, lakini hivi sasa linajadiliwa kuona namna ya kuwasaidia watahiniwa zaidi ya 240,000 waliopata ...