Tunaendelea na mada yetu tuliyoianza wiki kadhaa zilizopita juu ya makundi ya wanawake na mitazamo yao kwa wanaume. Baadhi ya wanawake wa kundi hili hulemaa kiasi cha kujifananisha na watu wazima. Hutokea mwanamke mwenye umri mdogo, kujiona ameshakuwa wa makamo kwa sababu tu ya aina ya wanaume ambao amekuwa akihusiana…
Hii ina maana kuwa wanawake wa aina hiyo wapo na wengi wao mwisho wake huishia kuwa akina mama wa nyumbani. Kwa ushauri wangu, mwanaume unapomsoma mwenzi wako yupo hivyo basi fanya jambo moja kati ya mawili. Mosi; Mrekebishe kama anarekebishika. Pili; Muache.
TATHMINI YA KIMAPENZI
Hawajui wala hawaheshimu hisia zao, neno mapenzi hulitafsiri katika kipengele cha chumbani tu, hususan kitandani. Kwao huwekeza zaidi nguvu zao kwenye kuhakikisha wanaume wao wanaridhika faragha na siyo kunako muktadha wa maisha ya uhusiano kwa jumla yake.
Ni kweli atajiweka safi na atahakikisha muda wote ananukia. Atavaa chachandu za kila aina kama vile shanga na cheni za kuvutia ili kumteka mwanaume aliyemlenga. Anaweza kutia fora kwa kununua nguo za ndani zenye sura tofautitofauti.
Atakuwa hodari kufanya mazoezi ya nyonga ili atishe kwa kuzungusha ‘bakuli’, kwa imani kwamba mwanaume anatekwa na uchakarikaji wa mwanamke kitandani. Vilevile hutaka afuzu mitindo, awe na uwezo mkubwa wa kubadili mikao wakati wa shughuli ya faragha.
Mwanamke wa aina hii, siyo mzuri sana kama utakuwa unataka mwenzi wa maisha yako, kwani yeye hataushughulisha ubongo wake kuhakikisha anaongeza pato la familia, badala yake hujielekeza kwenye eneo la kupata huduma za kimsingi.
Kundi hili ndilo ambalo huwa na wanawake wanaoitwa ‘magolikipa’. Yaani wale ambao husubiri wanaume waende kwenye mihangaiko, watafute riziki kisha wao waletewe. Mara nyingi hawana uamuzi wa kwao wenyewe, isipokuwa kila kitu huamuliwa na wanaume wao.
BAHATI MBAYA
Wanawake wa kundi hili hupoteza mvuto wao mapema, kwani hawataonekana wana jipya. Kwa vile ujanja wao upo kitandani, taratibu mapenzi ya wanaume hupungua kadiri wanavyozoeana. Mwisho humuona wa kawaida kwani hisia ni zilezile na mapenzi ni yaleyale.
Huonekana mzigo hasa pale wanaume wao wanapokuwa wanakabiliana na matatizo ya kiuchumi. Kwa kawaida, mume anapoona mambo magumu, huhitaji mwanamke ambaye anaweza kuisoma hali na kudhibiti matumizi.
Kadhalika, mwanaume hutaka kuwa na mwanamke ambaye anaweza kumpa mkewe kazi ya kugharamia chakula na matumizi madogomadogo ya nyumbani. Inapotokea mwanamke anakuwa hawezi kuingiza chochote, humtia kasoro katika harakati za maendeleo ya kimaisha.
Tatizo lingine ni kwamba inawezekana mwanamke akawa anajishughulisha lakini kwa sababu yeye anapenda kuhudumiwa, atahakikisha kipato chake anakibania ili aweze kutumia rasilimali za mwanaume peke yake.
Itaendelea wiki ijayo.
GPL
No comments:
Post a Comment