Friday, February 1, 2013

MAMA SHARO MILIONEA AMTOSA MTOTO ANAEDAIWA NI WA SHARO

MAMA wa aliyekuwa msanii wa muziki na filamu Bongo, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefungukia gari aliloacha mwanaye pamoja na mimba ambayo inadaiwa ni yake. 
Akizungumzia suala la gari, Mama Sharo amesema: “Kuhusu gari lile Toyota Opa aliloacha marehemu mwanangu naliuza kwani siwezi kuliendesha na haliwezi kukaa bila kufanya kazi yoyote.
“Kwa upande wa Marry Lucas wa Sumbawanga msichana aliyejitokeza baada ya Sharo kufariki na kusema ana ujauzito wake, siwezi kumtambua kwa sababu enzi za uhai Sharo hakuniambia kuwa ana mchumba wala mpenzi.”
Sharo Milionea alifariki dunia Nov 26, mwaka jana kwa ajali ya gari iliyotokea mkoani Tanga.
Siku chache baadaye, Marry aliibuka na kudai alikuwa mpenzi wa Sharo na ana ujauzito wake.

1 comment:

Anonymous said...

Huu ni unyama! Mama fanya Partenity test - DNA test kuhakikisha huyo si mjukuu wako. Ni bora iwe positive angalau utakuwa umeachiwa mjukuu na mwanao! Madaktari tujulisheni wapi unaweza fanya hii test ya kuconfirm kuwa huyu mtoto ni wake??