Meli ya kivita ya kupambana na uharamia aina ya Anti Submarine iitwayo Marshal Shaposhnikov’, ilipokuwa ikiingia na kasha baadae kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, kwa ziara fupi yenye lengo la kuimarisha urafiki baina ya Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na Urusi.
Wakati nchi ya Somalia ikiendelea kuwa kitovu cha uharamia, jumuiya ya kimataifa ilikubaliana kudhamiria kupambana na vitendo hivyo viovu. Lakini hadi sasa, wakati nchi nyingine zikitumia mbinu mbalimbali katika mapambano hayo, ni nchi za Russia, India na China pekee zinazosindikiza meli zao za biashara na nyinginezo ili kuzilinda na uharamia.
Meli hiyo imewasili siku ya Jumamosi na inategemea kuondoka kesho, Jumatano.
Balozi wa Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh akipokea salamu kutoka kwa kiongozi mkuu Rear Admiral Vladimir Vdovenko wakati alipotembelea meli hiyo bandarini.
Balozi Rannikh akiambatana na kiongozi wa wanajeshi waliofatana na meli hiyo Rear Admiral Vdovenko
Kwa pamoja, Balozi Rannikh na wanajeshi wa Kirusi waliimba wimbo wao wataifa wakiwa katika meli.
Balozi Rannikh akiwapongeza wanajeshi wake kwa kufika Dar es Salaam, Tanzania na kuwakaribisha nchi pia.
Baada ya salamu hizo, Balozi Rannikh nae alikaribishwa keki na mmvinyo iliyoandaliwa na wanajeshi katika meli.
Wanajeshi wa Kirusi wakionesha umahili wao wa ukakamavu muda mfupi kabla Balozi wan chi yao Mheshimiwa Rannikh hajapita mbele yao.
No comments:
Post a Comment