ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 21, 2013

Mmoja ajinyonga, mwingine anyongwa

Absalom Mwakyoma 
 Watu wawili wamekufa mmoja kwa kunyongwa na mwingine kujinyonga mwenyewe baada ya kubaini kuwa amefanya kosa la kuua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma, akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, alimtaja mtu aliyenyongwa kuwa ni Sabina Dominic (21), mkazi wa Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.

Kamanda Mwakyoma alisema kuwa Sabina alikuwa mfanyakazi wa ndani nyumbani kwa mfanyabiasha mmoja wa mafuta mjini hapa wakati aliyejinyonga ni Magesa Mathias, ambaye alichukua uamuzi huo baada ya kumnyonga mfanyakazi wake.Kamanda Mwakyoma alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 12:20 jioni nyumbani kwa Magori Chacha wakati mfanyakazi huyo akiwa nyumbani peke yake na wengine wakiwa kazini.

Alisema siku ya tukio aliingia nyumbani kwa kaka yake na kumkuta mfanyakazi huyo (Sabina) akiwa peke yake na kumfanyia unyama wa kumnyonga kwa kutumia pazia na kisha kumfunika na magodoro katika chumba cha kuhifadhia vitu mbalimbali.

Aliongeza kuwa chanzo cha mauwaji hayo bado hakijafahamika na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

CHANZO: NIPASHE

No comments: