Wednesday, February 6, 2013

MONALISA NA RIYAMA WATOANA JASHO LA UHAKIKA


Actresses maarufu wa Swahiliwood Riyama Ally na Yvon Cheryl (Monalisa) wameonekana kuingizwa katika mpambano usio rasmi hivyo kutoana jasho la uhakika katika kumtafuta muigizaji anayeuvaa uhusika vizuri katika filamu. Hayo yametokea Facebook katika page ya East Africa Radio kwa kuandika hivi "
Unadhani kati ya mabinti hawa nani huwa anavaa uhusika halisi anapoigiza na anafaa kuvikwa taji la 'Bongo Movies Queen'.
Riyama ally V/S Yvonne Cherry (Monalisa)". wachangiaji zaidi ya 2000 wamechangia na kila shabiki akimtaja aidha Monalisa au Riyama kuwa bora na mpambano huo kuwa mkali hasa maana mashabiki wameonekana kuhamasika sana kumjua mshindi kati ya waigizaji hao wenye vipaji. Tofauti na baadhi ya waigizaji wengine wanapopambanishwa husifiwa kwa uzuri wa sura zao au maumbo lakini ni tofauti kwa Monalisa na Riyama ambao licha ya kuwa warembo silaha yao kubwa kwa mashabiki ni vipaji vyao.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake