Wednesday, February 6, 2013

TAIFA STARS YAIFUMUA CAMEROON 1-0

Shujaa wa Stars leo, Samatta

Na Mahmoud Zubeiry
MBWANA Ally Samatta, jioni hii ameibuka shujaa wa taifa, baada ya kuifungia Tanzania, Taifa Stars bao pekee la ushindi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Cameroon Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mpira uko nyavuni, Samatta anachomoka kushangilia
Aminou Bouba wa Cameroon (kulia), akijaribu kuudhibiti mpira huku akikabwa na Erasto Nyoni (4) wa Taifa Stars katika mchezo huo. Stars imeshinda bao 1-0 lililofungwa na mchezaji wa kimataifa Mbwana Samatta baada ya kupata pasi ya Erasto Nyoni katika dakika ya lala salama ya 89.
Mashabiki wa Taifa Stars wakifuatilia mchezo huo.
Dakika ya 89 Mbwana Samatta, ameipatia Taifa Stars bao akimalizia pasi ya Erasto Nyoni.
Taifa Stars ingepata magoli mengi katika mchezo huo, lakini Kutokuwa makini kwa wachezaji frank domayo na amri kiemba, kumeikosa stars bao zuri baada ya kupiga mpira nyongo uliyopaa juu, ikiwa dakika ya 82 ya mchezo.
Taifa Stars; Juma Kaseja, erasto nyoni, shomary kapombe, kelvin yondani, agrrey morris,abubakar salum, mrisho ngassa, frank domayo, mbwana samanta, mwinyi kazimoto na amri kiemba.
Cameroon effala komguep, assou ekottob, aminou bouba, nyom allan, pirre wome nlend, kigue mpondo, bedimo herny, tchami herve, olinga fabrice,aboubakar vincent, ngoula patrick. Mwisho
Mpaka mapumziko si stars wala cameroon iliyopata bao. Dakika ya 25 boubakary vicent alipiga shuti hatari kwa Stars, But alipiga pembeni na kuikosesha cameroon bao.
Dakika ya 27 Erasto Nyoni amekosa penati na kuinyima stars bao la kuongoza, baada ya kupanguliwa na kipa wa cameroon. Dakika ya 9 Mwinyi Kazimoto alipiga shuti lakini kipa cameroon akadaka.

1 comment:

  1. Binafsi maoni yangu yamegawanyika sehemu kubwa mbili.
    Sehemu ya kwanza ni kuhusu timu yetu. Tumeshuhudia tukiwafunga waliokuwa mabingwa Zambia na sasa tumewafunga Cameroon kweli ni matokeo yanoyotia moyo. Kweli inatia moyo walau sasa tunaweza kufanikiwa kufika mbali kama juhudi zikiongezwa na kila mmoja kwa nafasi yake akafanya wajibu wake ipasavyo hiyo ni kwa Viongozi, wachezaji, washabiki yaani kwa ujumla wadau wote tuwajibike kuisapoti timu.

    Suala la pili ni kuhusu huyu muandishi aliyetuandikia hii taarifa. Kweli tunashukuru mtandao huu kwa kutupa habari za nyumbani kwa haraka kuliko hata mitandao ya magazeti au vyombo vingine vya habari. Lakini hii habari jinsi ilivyoandikwa ni kana kwamba mtu alikuwa na haraka akaamua aandike tuu ili afanye kitu kingine kwani habari haijaandikwa kwa ufasaha. Tulitegemea walau muandishi atuelezee hali ya mchezo ilikuwaje, makocha waliongeleaje kuhusu mechi hiyo. Yaani tusome habari kiasi sisi tusiokuwa uwanjani tunapata taswira ya kile kilichotokea.
    Samahani ndugu muandishi kama nimekukera lakini huo ni mtazamo wangu tuu, pia nashukuru kwa taarifa ya mchezo uliyotupatia kwani mimi binafsi nilikuwa naisubiria kwa hamu sana.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake