Monday, February 4, 2013

MPANGO WA USAFIRI HURIA WA ANGA EAC UNAENDELEA VIZURI

Na Mwandishi wa EANA
Arusha, 5 Februari,2013 (EANA) Afisa Mkuu Mwandamizi wa Msuala ya Anga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Ladislaus Matindi amesema mchakato wa usafiri huria wa anga katika kanda ya ya EAC unaendelea vizuri na kwamba jumuiya inatarajiwa kuuchambua mswada husika mwishoni mwa Mei, mwaka huu.
‘’Kutokana na maendeleo yaliyopo, inatarajiwa kwamba operesheni ya kuleta tija na kuongeza fmasafa na uwezo litatuongoza katika hatua ya juu ya utoaji huduma katika soko ya anga katika kanda na pia kupunguza nauli na gharama za kusafirisha mizigo,’’ alithibitisha Matindi.
Mapema mwaka 2006, Mkutano wa 11 wa Baraza la Mawaziri la EAC lilifanya mabadiliko makubaliano yaliyopo ya Usafiri wa Anga (BASAs) baina ya nchi kuhusu kuondoa vikwazo vya uwezeshwaji na masafa , kuwa ni hatua za awali kabisa katika utekelezaji wa mpango huo.
Matindi aliendelea kusema kuwa eneo la kuanzia kwa EAC katika juhudi zake za kuanzisha usafiri huria katika soko la anga ni uamuzi wa baraza la mawaziri kuhusiana na utekelezaji wa azimio la Yamoussoukro la Oktoba 7, 1988 juu ya kufanya usafiri wa anga katika soko la Afrika kuwa huria, jambo ambalo halijatekelezwa.
Afisa huyo wa EAC alirudia kwamba kwa kuzingatia utekelezaji wa azimio hilo katika kanda ya EAC na matumizi ya makubalino ya Soko la Pamoja, nchi wananchama wa EAC zitaweza kuiondoa zenyewe vikwazo dhidi ya maendeleo ya sekta ya anga vinavyohusiana na uwezo, masafa,uhujumu na uchaguzi wa makampuni ya ndege.
Alisema changamoto ambayo ya wazi kabisa ni ya uhakika kuwepo kwa biashara ya ushindani uliosawa kati ya kampuni ndogo za usafiri wa anga na makubwa .

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake