Monday, February 4, 2013

WAFUASI WA CHADEMA NA CCM MKOANI DODOMA WAGOMBANIA ENEO NA MTI WA KUTUNDIKA BENDERA ZAO.

Mbunge wa Tabora Mjini(CCM)ismail Aden Rage(wa pili Kulia aliyeshika bomba)akipambana na vijana wa chadema eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.
Kada wa Chadema Mkoani Dodoma, Arnold Swai akipokonywa mti wa bendera ya chadema na wafuasi wa CCM jana, baada ya kutokea vurugu katika eneo la Mwanga baa, Dodoma 
Mmoja wa Wafuasi wa Chadema akishikwa na polisi baada ya wafuasi wa CCM na Chadema Kugombea eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.Picha Zote na Mpoki Bukuku
--
SHEREHE za miaka 36 za kuzaliwa kwa CCM jana ziliingia dosari, baada ya kuibuka vurugu kubwa kati ya wafuasi wa chama hicho na Chadema mkoani Dodoma wakati wakigombea eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.
Vurugu hizo zilizotulizwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), zilitokea jana mchana katika uwanja huo uliopo karibu na Baa ya Mwanga, baada ya CCM kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwepo uwanjani hapo, ili waweke bendera zao kwa ajili ya mkutano ambao ulikuwa sehemu ya maadhimisho hayo.
Vurugu zilizuka baada ya wafuasi wa Chadema kuwataka wenzao wa CCM waendelee na mkutano katika eneo hilo kwa sharti la kurejeshwa kwa bendera iliyong’olewa. Wafuasi wa vyama hivyo wakiwamo wabunge wa CCM walionekana wakivutana kunyang’anyana mti wa bendera.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake