ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 18, 2013

SALA YA KUMUOMBEA NA KUMKUMBUKA MZEE KOMBE, DMV


Mchungaji Ferdinand Shideko akiendesha Sala ya kumuombea na kumkumbuka Marehemu Mzee Kombe aliyefariki December 14, 2012 nyumbani kwake Lanham, Maryland, nchini Marekani na kuzikwa nyumbani Kilema, Moshi, Tanzania Sala ilifanyikia College Park, Maryland, Jumapili Feb 17, 2013.

Mke wa Marehemu Mrs Mary Kombe akiongea machache kuwashukuru wote kwa kuwa kwao karibu na familia wakati wote tangia kuugua hadi kufariki kwa marehemu. Mrs Mary Kombe aliendelea kusema ukaribu huo umewafanya kutojisikia upweke wa kuondokewa na mpendwa na nguzo ya familia yao kusema ukweli tumefarijika sana.

Flora Mkande akiongea jambo

Watanzania wa DMV waliojumuika pamoja wakiongozwa na mkuu wa utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka (wa kwanza kushoto)

Familia ya Mzee Kombe ikiwa kanisani College Park kwenye sala ya kumuombea na kumkumbuka mpendwa wao

Juu na chini ni Watanzania wa DMV waliojumuika pamoja na familia kwenye sala ya kumuombea na kumkumbuka Mzee Kombe iliyofanyika Jumapili Feb 17, 2013 College Park, Maryland nchini Marekani.

Kwaya ya nyimbo za Injili ikiimba kwenye sala ya kumuombea na kumkumbuka Mzee Kombe

Juu na chini ni Watanzania wa DMV wakitoa mkono wa pole kwa Mrs Mary Kombe na wanafamilia baada ya sala ya kumuombea na kumkumbuka Mzee Kombe kumalizika
Kwa picha zaidi bofya read more






No comments: