Tuesday, February 5, 2013

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWA UONGOZI WA PPF

TAARIFA KWA UMMA
Tunasikitika kuwataarifu kwamba mnamo tarehe tatu mwezi wa pili mwaka elfu mbili na kumi na tatu(3/02/2013) saa kumi na mbili asubuhi(12:00) kulitokea ajali ya moto katika chumba cha mifumo ya mawasiliano kilichopo sehemu ya juu kabisa Jengo la PPF Tower lililoko makutano ya mtaa wa Ohio na Garden Avenue.
Moto huo ulidhibitiwa kwa ushirikiano wa vikosi mbalimbali vya zima moto. Zoezi hilo la uzimaji wa moto lilitumia kiasi kikubwa cha maji ambayo yalisambaa kwenye maeneo ya ngazi,mifumo ya umeme na mawasiliano.
Wataalamu wanaoshughulikia mifumo ya umeme katika jengo wamefanya ukaguzi na kushauri kusitishwa kwa matumizi ya umeme katika jengo hilo mpaka watakapokamilisha zoezi la ukaushwaji wa maji hayo. 
Zoezi hilo linatarajiwa kukamili mapema iwezekanavyo.
Moto huo haukuathiri sehemu nyingine za jengo hilo zikiwemo ofisi za wapangaji.
Tunaomba uvumilivu kwa wapangaji na watumiaji wa jengo wakati zoezi la ukaushaji wa maji hayo na kisha kuwasha umeme linaendelea.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake